Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma akimkabidhi laptop Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Kimara, Mhe. Asia Mj...
Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma akimkabidhi laptop Hakimu
Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Kimara, Mhe. Asia Mjemah kwa ajili ya
uchapishaji nakala za hukumu jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma akizungumza katika
ufungaji wa maonesho ya wiki ya sheria katika viwanja vya Mnazi mmoja
jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya viongozi mbalimbali na wananchi wakimsikiliza Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania Profesa Ibrahimu Juma katika ufungaji wa maonesho ya wiki ya
sheria katika viwanja vya Mnazi mmoja jana jiji Dar es Salaam
Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa,Ibrahimu Juma akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi mblimblia katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jiji
Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mahakama
kuu ya Tanzania imesema itafanya mpango wa kuongeza kasi ya utoaji wa
haki kwa watu wote ikiwemo kupunguza kesi za zamani katika ngazi zote
za mahakama nchini.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa
Ibrahim Hamis Juma katika kilele cha maonyesho ya wiki ya sheria,
akisisitiza watongeza vitendea kazi na watumishi wa mahakama ili kuwepo
na urahisi katika mfumo wa kusikiliza kesi na kuzitolea hukumu.
Akizungumzia
baadhi ya malalamiko yaliyotolewa na mmoja wa wananchi Profesa Juma
amesema kuwa wamepokea malalamiko juu ya mahakama moja ambayo hakuitaja
jina lake ambayo watumishi wake wamekuwa wakitoa lugha
chafu,uzembe,kuchelewesha haki,kutumika kama vishoka sambamba na kuongea
lugha za jazba hali ambayo ilimkwaza mwananchi huyo.
‘’Natoa
rai kwa mahakama kuhakikisha wanatoa takwimu nawakumbusha kwamba kuna
waraka wa Jaji Mkuu wa mwaka 2013 ambao aliwataka Majaji
wafawidhi,Majaji wafawidhi na watendaji kuona kila baada ya miezi mitatu
kuanzia Julai 2013 kuwasilisha mashauri ya muda mrefu’’. amesema
Profesa Juma.
COMMENTS