Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka wachimbaji mchanga na walima bustani za...
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba amewataka wachimbaji mchanga na walima bustani za mbogamboga katika bonde
la mto Msimbazi katika kata Vingunguti iliyopo katika Manispaa ya
Ilala, kuondoka mara moja na kuacha shughuli hizo.
Ameyasema
hayo alipokua katika ziara ya siku moja ya kutembelea kata ya
Vingunguti na kujionea athari mbalimbali za mazingira katika kata
hiyo.
Wakiongea
mbele ya Waziri Makamba, Wananchi wamelalamika kero mbalimbali
zinazowakabili ikiwemo bonde hilo kuzidi kumong'onyoka na kusogelea
makazi ya watu pamoja na eneo la makaburi.
Hivyo
basi kusababisha nyumba zao kuanguka na makaburi kumong'onyoka hali
amabayo inahatrisha maisha yao na kuwafanya kuishi kwa hofu.
Akijibu
kero hiyo Waziri Makamba aliwaambia kuwa atayafanyia kazi maombi yao na
atakaa na viongozi wa Manispaa na wa Ofisi yake ili kupata suluhu ya
matatizo yao.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akiangalia bonde la mto Msimbazi katika kata ya Vingunguti
lilivyoharibika kwa shughuli za kila siku za Wananchi ikiwemo kilimo cha
mbogamboga na uchimbaji wa mchanga. Waziri Mkamba yupo katika ziara
kutembelea kata ya Vingunguti kukagua athari za mazingira.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba pamoja na Mbunge wa jimbo la Segerea Mh. Bonnah Klauwa
wakiskiliza kero mbalimbali zinazotolewa ana Wananchi wakati Mh. Waziri
alipofanya ziara katika kata ya Vingunguti kukagua athari mbalimbali za
mazingira.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akiongea na Wananchi waliojikusanya kumsikiliza wakati wa ziara
yake katika kata ya Vingunguti katika wilaya ya Ilala jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akipata maelezo, toka kwa vijana wa kata ya Vingunguti juu ya
utenegenezaji wa majiko ya mkaa ambayo ni rafiki wa mazingira na ambayo
hayatumii mkaa mwingi.
COMMENTS