JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO Simu ya Upe...
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo: DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM, 07 Februari, 2017.
Tele Fax : 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu uvaaji wa sare za Jeshi kwa viongozi wanajeshi wanaoteuliwa na kupewa madaraka mbalimbali nje ya Jeshi. Hivi karibuni kumekuwa na mjadala juu ya uhalali wa uvaaji wa sare hizo.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kuwataarifu wananchi kuwa kulingana na kanuni za Majeshi ya Ulinzi juzuu ya kwanza, viongozi hao wanaruhusiwa kisheria kuvaa sare za Jeshi wanapokuwa wakitekeleza majukumu maalum, hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa viongozi hao waliopo katika maeneo yao.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085.
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo: DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM, 07 Februari, 2017.
Tele Fax : 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Mhe:Dkt John Pombe Joseph Magufuli amewaapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali James Aloyce Mwakibolwa. Katika sherehe hizo vyombo vya habari vilishiriki kikamilifu kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi na kwa wakati.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa shukrani za dhati kwa vyombo vyote vya habari kwa kushirikiana na Jeshi katika tukio hilo muhimu la kihistoria kwa nchi yetu, Jeshi linatambua na kuthamini mchango wa vyombo vya habari katika maendeleo ya Taifa letu, linaomba ushirikiano huu uendelee.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085
COMMENTS