WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WA UTAFITI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI
HomeJamii

WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WA UTAFITI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu y...

SISTER FLORA NDWATA ASHINDA TUZO ZA JUMLA ZA WANAWAKE WENYE MAFANIKIO TANZANIA (TWAA)
NAIBU WAZIRI MAVUNDE AENDELEA KUWABANA WAAJIRI WANAOKIUKA SHERIA ZA NCHI
WANAWAKE TAA WAUNGANA NA WENZAO MLIMANI CITY DAR ES SALAAM KUADHIMISHA SIKUKU YA WANAWAKE DUNIANI






Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.





NA VERONICA KAZIMOTO
WITO umetolewa kwa viongozi wa Serikali na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wadadisi watakaopita maeneo mbalimbali nchini kukusanya taarifa kwa ajili ya Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.


Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa utafiti huo yaliyofanyika leo mkoani Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ladislaus Mwamanga, (pichani juu), amesema utafiti huo ni muhimu katika kunusuru kaya maskini nchini hivyo haina budi viongozi na wananchi kutoa ushirikiano kwa Wadadisi wa utafiti husika.


"Kwa namna ya pekee nawaomba Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya, Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri, viongozi wa kata na vijiji na wananchi wote kwa pamoja mtoe ushirikiano wa hali ya juu kwa Wadadisi watakapokuwa katika maeneo yenu wakikusanya taarifa za utafiti huu", amesema Mwamanga.


Nae Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema lengo la kufanya mafunzo hayo ilikuwa ni kuwawezesha Wadadisi kufahamu taratibu zote zinazohusu kazi ya ukusanyaji taarifa na mbinu zinazotakiwa ili kupata taarifa sahihi kutoka kwenye kaya mbalimbali nchini.


Jumla ya Wadadisi 85 wamemaliza mafunzo ya siku 20 ya Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na TASAF.



Mmoja wa Wadadisi Maro D. Maro akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.



Baadhi ya Wadadisi na Wasimamizi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)






Baadhi ya Wadadisi na Wasimamizi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WA UTAFITI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI
WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WA UTAFITI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUZBsOy7EAZpHuzuNx3FpxhuM5p-zDd3RR8Qrak6hCk27Y9T68GwPzh-48Kuotl-QvZU8BEp849yGAFiU0N6U87m_23CLBPC7Enghf_klsbHGKmnzkxZBorR15HglOpwNMwoiQrvgZuqGA/s640/PICHA+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUZBsOy7EAZpHuzuNx3FpxhuM5p-zDd3RR8Qrak6hCk27Y9T68GwPzh-48Kuotl-QvZU8BEp849yGAFiU0N6U87m_23CLBPC7Enghf_klsbHGKmnzkxZBorR15HglOpwNMwoiQrvgZuqGA/s72-c/PICHA+1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/07/wito-watolewa-kwa-wananchi-kutoa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/wito-watolewa-kwa-wananchi-kutoa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy