WAZIRI MKUU AWAASA WATUMISHI WANAOFANYAKAZI VIWANDANI
HomeJamii

WAZIRI MKUU AWAASA WATUMISHI WANAOFANYAKAZI VIWANDANI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa  Mkutugenzi wa Ufundi, Bw. McJohn Mbiri  (kulia Kwake)  kuhusu mitam...

RAIS DKT. MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YAKE YA SH. MILIONI 60 KWA WAJUMBE WA CHAMA CHA WALIMU PAMOJA NA WANAFUNZI WA UDOM WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO CWT
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, ABDALLAH ULEGA AZ AKIZINDUA ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO
MIILI YA MASHUJAA WA TAIFA YAAGWA: NI WALE WANAJESHI 14 WA JWTZ WALIOUAWA DRC


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa  Mkutugenzi wa Ufundi, Bw. McJohn Mbiri  (kulia Kwake)  kuhusu mitambo ya kuzaisha gesi ya hewa ya ukaa wakati alipotembelea kiwanda cha TOL Limited  kilichopo katika kijiji cha Ikama wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
NA OWM, RUNGWE
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaofanya kazi katika viwanda mbalimbali nchini kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu.

Amesema Tanzania imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda hivyo ni vema watakaopata fursa ya ajira katika viwanda hivyo kuwa waadilifu.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 30, 2017) wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha gesi cha Ikama kilichoko wilayani Rungwe.

Waziri Mkuu amesema wakati Serikali ikiendelea kuwakaribisha wawekezaji nchini, wananchi walioajiriwa kwenye maeneo hayo wawe waaminifu.

“Mnatakiwa muwe waaminifu, msibebe kitu chochote ndani ya kiwanda bila ya ridhaa ya wamiliki kwa kuwa mtaonyesha taswira mbaya kwa wawekezaji.”

Amesema uaminifu wao ndio utawezesha Watanzania wengi kupata ajira kwenye viwanda hivyo ambavyo vimejengwa  katika maeneo yao.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya TOL Gases, Mhandisi  Harold Temu alisema kiwanda kinauwezo wa kuzalisha tani 46 kwa siku.

Alisema gesi inayozalishwa kiwandani hapo ni ya Carbon Dioxide ambayo inauzwa nchini na nchi jirani za Zambia, Malawi, Zimbabwe na Congo.

Mhandisi Temu alisema wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda vya kutengenezea soda, bia na pia hutumika katika kuhifadhia chakula na kwenye vifaa vya kuzimia moto.

Mapema Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kuchakata majani ya chai cha Katumba, ambapo alisema Serikali inaimarisha Ushirika wa zao hili ili wakulima waweze kupata tija.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitembelea kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya  Amos Makalla na kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Ramadhani Kampasili.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitazama  chai iliyosindikwa na kufungashwa tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea kwianda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa kiwanda cha gesi cha TOL Gasese Limited kilichopo katika kijiji cha  Ikama wilayani Rungwe Baada ya kuwasili kiwandani hapo Julai 30, 2017 Kushoto ni Naiobu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana viongozi wa kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rung wakati alipowasili kiwandani hapo kukagua shuguli za kiwanda hicho Julai  30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Rungwe baada ya kutembelea kiwanda cha Chai cha Katumba Julai 30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya asili baada ya kuwasili kwenye uwanja wa michezo wa Kandete  katika jimbo la  Busokelo mkoani Mbeya kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 30, 2017.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Busokelo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa michezo wa Kandete katika jimbo la Busokelo kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 30, 2017.(PICHA NA OWM)

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AWAASA WATUMISHI WANAOFANYAKAZI VIWANDANI
WAZIRI MKUU AWAASA WATUMISHI WANAOFANYAKAZI VIWANDANI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjI5jeP_agYZQzu0Itv-PUTPVvNgYcgAaq9tdf2u8FtecejZajFEoKFSBs3X5IYVtzyU5ICL4mSEsDwNe96KlDXfmuvHYBqi-kvUQ9ocgRd1CHDAZkrxEfp-HuvL21q5BGb_Rn2wH9HhQkc/s640/PMO_6809.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjI5jeP_agYZQzu0Itv-PUTPVvNgYcgAaq9tdf2u8FtecejZajFEoKFSBs3X5IYVtzyU5ICL4mSEsDwNe96KlDXfmuvHYBqi-kvUQ9ocgRd1CHDAZkrxEfp-HuvL21q5BGb_Rn2wH9HhQkc/s72-c/PMO_6809.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/07/waziri-mkuu-awaasa-watumishi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/waziri-mkuu-awaasa-watumishi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy