TAARIFA YA SERIKALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO
HomeJamii

TAARIFA YA SERIKALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IDARA YA HABARI-MAELEZO                          SERIKALI YAFAFANUA SHEREHE ZA MUUNGANO, GESI NA UE...

WAZIRI JAFO:SITAKI UKANJANJA KATIKA UJENZI WA STENDI YA MABASI MBEZI LUIS
TANZANIA YATAJWA KUWA BUSTANI YA EDEN NA CHIMBUKO LA MWANADAMU WA KALE DUNIANI
RAIS DKT. MAGUFULI AONGEA NA WANANCHI MIKUMI, AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA KIDATU –IFAKARA YENYE KM 66.9 NA DARAJA LA MTO RUAHA ENEO LA NYANDEO KIDATU
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

IDARA YA HABARI-MAELEZO

                        

SERIKALI YAFAFANUA SHEREHE ZA MUUNGANO, GESI NA UENDESHAJI WA MICHEZO YA BAHATI NASIBU


Dodoma, Jumatano, 8 Februari, 2017:  


Serikali imefafanua kuhusu sherehe za Muungano, manufaa na kiasi cha gesi nchini na utaratibu wa michezo ya bahati nasibu hapa nchini. Ufafanuzi huo umetolewa leo mjini hapa.


Zuio la Sherehe za Muungano


Serikali imefafanua kuwa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa mwaka 2016 yalifanyika kwa wananchi kupumzika siku hiyo na kuendelea kutafakari umuhimu wa Muungano. Alisema wananchi waliadhimisha kwa kufanya shughuli anuai kama vile usafi wa mazingira na kujitolea katika shughuli mbalimbali za maendeleo.


Akifafanua kuhusu hoja hiyo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde amesema si kweli kwamba sherehe hizo zilizuiwa na akaongeza kuwa Serikali haina kumbukumbu zozote za watu binafsi walioingia hasara kwa kufanya maandalizi ya sherehe hizo.


Kiasi cha Gesi Nchini


Serikali imesema kuwa gesi asilia iliyogunduliwa katika maeneo ya baharí ya kina kirefu ni futi za ujazo trilioni 47.08 na katika nchi kavu ni futi za ujazo trilioni 10.17, hivyo nchi kuwa na jumla ya futi za ujazo trilioni 57.25 za gesi asilia. Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema gesi iliyogunduliwa nchini na safi ikiwa na kiwango kidogo cha kemikali ya alfa.


Ameongeza kuwa moja ya manufaa ya gesi hiyo ni uzalishaji wa umeme ambapo mpaka sasa uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia umeongezeka kutoka uniti 2,714.25 milioni kwa mwaka 2014 hadi uniti 4,196.4 milioni mwaka 2016 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 54.61.


Aidha, amesema kutokana na unafuu wa umeme wa gesi, bei ya umeme imeshuka kutoka wastani wa shilingi 188.56 kwa uniti mwaka 2014 hadi wastani wa shilingi 125.85 kwa uniti mwaka 2016 sawa na punguzo la asilimia 33.26.

Ongezeko la Maduka ya Kucheza Kamari


Serikali imefafanua kuwa, michezo yote ya kubahatisha ikiwemo kamari inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Namba 4 ya mwaka 2003, Sura 41 pamoja na Kanuni zake. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kwa mujibu wa Sheria, hakuna mtu au taasisi inayoruhusiwa kuendesha biashara ya Michezo ya Kubahatisha bila kuwa na leseni kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha.


Dkt. Kijaji ameongeza kuwa Sheria pia inakataza watoto wenye umri chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia, kukaa au kuzurura karibu na maeneo ya michezo ya kubahatisha. Ameasa kuwa, mtu yeyote atakaye ruhusu mtoto chini wa miaka 18 kushiriki, kuingia au kukaa karibu na eneo la mchezo wa kubahatisha anahesabuka kufanya kosa na anastahili kulipa faini ya sh. 500,000 au kifungo kisichopungua miezi mitatu ama vyote kwa pamoja.


Imetolewa na:


Idara ya Habari-MAELEZO.



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

IDARA YA HABARI-MAELEZO

                        



SERIKALI YAAINISHA MIKAKATI, UTEKELEZAJI KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA


Dodoma, Jumatano, 8 Februari, 2017:  


Serikali imeainisha muelekeo wa utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda na kufafanua masuala mengine mbalimbali kuhusu uhifadhi wa mazingira, uwekezaji, na uendeshaji wa mashirika ya umma. Ufafanuzi huo umetolea jioni hii wakati wa kujibu hoja za wabunge na maoni ya Kamati za Kudumu za Bunge za Viwanda, Biashara na Mazingira na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.


Tanzania ya Viwanda


Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage amesisitiza kuwa Serikali imeanza kupata mafanikio katika utekelezaji wa mkakati wake wa kufikia Tanzania ya Viwanda. Wakijibu hoja mbalimbali jioni hii, Waziri Mwijage na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango, wamesema ingawa Serikali haijengi viwanda moja kwa moja lakini imeendelea kuweka mazingira mazuri kuhakikisha viwanda vinashamiri nchini.  


Waziri Mwijage amesema kutokana na uwezeshaji huo wa Serikali tayari kuna miradi zaidi ya 1,169 ya viwanda iliyokwisha sajiliwa kupitia taasisi mbalimbali kama Kituo cha Uwekezaji (TIC), Mamlaka ya Kusimamia Kanda Maalum za Kiuchumi (EPZA), Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO).


Alisema katika miradi hiyo ipo ambayo inakaribia kukamilika ikiwemo kiwanda cha vigae kilichoko Mkuranga, Pwani na uwekezaji katika kiwanda cha Tamco, Kibaha, Pwani ambako kazi ya kuunganisha matrekta yapatayo 2,400 itafanyika kufikia mwishoni mwa mwaka huu.   


Naye Waziri wa Fedha, Dkt. Mpango amesisitiza Serikali itaendelea kuhakikisha utekelezaji wa viwanda na imetenga fedha kwa ajili ya kusaidia na kurahisisha uwekezaji huo. Amesema pia Serikali itaendelea kujenga miundombinu kama vile kuboresha upatikanaji wa umeme, usafirishaji na kuhamasisha wawekezaji kwa kuwapatia mazingira mazuri ya kufanya biashara.


Akichangia hoja hiyo, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amesema nishati ya umeme ni muhimu kwa uwekezaji wa viwanda na kutoa ushauri kwa wawekezaji wanaotaka kujenga viwanda popote nchini wasiende kimya kimya, watoe taarifa ili wizara yake iwaunganishie nishati hiyo haraka.


Mikataba Mibovu


Kwa upande wa malalamiko ya wabunge kuwa kuna baadhi ya mikataba iliyoingiwa na baadhi ya taasisi hapa nchini kuwa ni mibovu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, amezishauri Wizara zenye taasisi kama hizo ziitumie ofisi yake kupata ushauri wa namna ya kupitia upya mikataba hiyo.


Fedha Zaidi Uhifadhi Mazingira


Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba na Naibu wake, Luhaga Mpina wameeleza hatua mbalimbali za kuhifadhi mazingira nchini na changamoto zake. Waziri Makamba amekiri kuwa hali ya mazingira nchini inahitaji uwekezaji mkubwa ili kuliokoa Taifa na majanga mbalimbali. Amelipa changamoto Bunge kuhakikisha kuwa miradi ya mazingira inapewa bajeti ya kutosha.


“Wengi hapa mmezungumzia changamoto nyingi za mazingira, Nikiri kuwa ni kweli hali ya uhifadhi wa mazingira ni mbaya sana. Sasa naomba kurudisha changamoto hii kwenu; Bunge lione namna ya kuhakikisha kunapangwa fedha za kutosha ili zitumike kwa ajili ya miradi ya hifadhi ya mazingira,” alisema.


Imetolewa na:


Idara ya Habari-MAELEZO.





Bunge jana liliketi kikao chake cha sita katika mkutano wa Sita wa Bunge la 11 mjini Dodoma. Mbali na kipindi cha Maswali na majibu lakini pia Wabunge walipokea taarifa za Kamati mbili za Kudumu za Bunge ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya na Ile ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Pichani juu ni Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdul Aziz Abood akiuliza swali Bungeni Mjini Dodoma jana kuhusiana na masuala ya usambazaji umeme katika baadhi ya vijiji klatika jimbo lake.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano Mh. Luhaga Mpina akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma ambayo yalielekezwa katika Wizara yake. 
 Mbunge wa Konde Zanzibar, Khatib Said Haji akiuliza swali kwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Bungeni mjini Dodoma jana juu ya masuala ya ucheleweshaji wa kesi mbalimbali kutokana na ucheleweshaji wa upelelezi jambo linalosababisha kuwepo na ongezeko kubwa la mahabusu Magerezani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akijibu swali la Mbunge wa Konde Khatib Said Haji pamoja na maswali mengine ya nyongeza.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harison Mwakyembe akisaidia kujibu maswali yaliyoelekezwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambayo yalihitaji ufafanuzi wa kina wa kisheria na hasa pale yalipozungumza mambo yanayohusiana na Ugaidi.
 Mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul akiuliza swali Bungeni.
 Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati akiuliza swali Bungeni.
 Wabunge wakifuatilia mjadala wa Bunge mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani akijibu maswali yaliyoulizwa katika Wizara yake.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medad Kalemani (kulia) akizungumza jana na Mbunge wa Morogoro Mjini Bungeni mjini Dodoma  
 
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Kagera,  Oliver  Semuguruka Bungeni mjini Dodoma.


 Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson akizungumza na Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby Bungeni mjini.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAARIFA YA SERIKALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO
TAARIFA YA SERIKALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO
https://lh3.googleusercontent.com/1IuDb6JnwHpYDVqqPRDTTtR7tGEfn3x0Q4UVd-b0x5vwFtI0kwzASY2Xg4RyaIAY4toQpYAxBMCB6x1uHKe4odZ2pFCEcCVooVXDVTZAHZi_XT4PRtFv3eHyewo3SV0Jj2oaVhS9d8UtIoWjpg
https://lh3.googleusercontent.com/1IuDb6JnwHpYDVqqPRDTTtR7tGEfn3x0Q4UVd-b0x5vwFtI0kwzASY2Xg4RyaIAY4toQpYAxBMCB6x1uHKe4odZ2pFCEcCVooVXDVTZAHZi_XT4PRtFv3eHyewo3SV0Jj2oaVhS9d8UtIoWjpg=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/taarifa-ya-serikali-kutoka-bungeni.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/taarifa-ya-serikali-kutoka-bungeni.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy