WAZIRI JAFO:SITAKI UKANJANJA KATIKA UJENZI WA STENDI YA MABASI MBEZI LUIS
HomeJamii

WAZIRI JAFO:SITAKI UKANJANJA KATIKA UJENZI WA STENDI YA MABASI MBEZI LUIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Viongozi wa mkoa wa Dar es salaam na w...

VIJANA WA CHUO CHA KODI NI HAZINA KWA FAIDA- TRA
RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MAJENGO YA HOSTELI ZA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
MIILI YA ASKARI NANE WALIOUAWA NA MAJAMBAZI MKOANI PWANI YAAGWA RASMI,WAZIRI MWIGULU ATANGAZA KIAMA KWA WATUHUMIWA






Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Viongozi wa mkoa wa Dar es salaam na wilaya ya Ubungo katika ukaguzi wa eneo la ujenzi wa Stendi ya Mbezi Luis.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akikagua mipaka ya eneo la ujenzi wa Stendi ya Mbezi Luis.

Viongozi mbalimbali wakisikiliza maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo kuhusu ukaguzi wa eneo la ujenzi wa Stendi ya Mbezi Luis.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akipata maelezo ya eneo linalotarajiwa kujengwa stendi ya mabasi ya kisasa ya Mbezi Luis.
............................................................
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewaonya watu ambao ni makanjanja wa miradi ya maendeleo kwamba hatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria huku akisema hatarajii kuwaona katika mradi wa stendi ya mabasi ya mikoani inayotarajiwa kujengwa Mbezi Luis jijini Dar es salaam.


Jafo ameyasema hayo alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa stendi hiyo eneo la Mbezi Luis jiji Dar es salaam.


Ujenzi wa stendi hiyo unatarajiwa kuanza kujengwa miezi michache ijayo baada ya jiji la Dar es salaam kupata fedha Sh. bilioni 50 kutoka serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI.


Akizungumza katika eneo hilo, Jafo amesema kuna baadhi ya watu wanapoona miradi mikubwa kama hiyo huwa wanapanga mikakati ya kuhujumu au kujipatia fedha kwa kufanya ufisadi.


"Wataofanya hivyo waelewe wazi hawatabaki salama," Amesisitiza Waziri Jafo


Aidha, Jafo amesisitiza kauli ya Rais Dk. John Magufuli aliyoitoa wakati akizindua stendi ya mabasi ya Msamvu kwamba katika ujenzi wa stendi zote lazima zizingatie mahitaji ya wadau mbalimbali hususan Mama na baba Nitilie ili waweze kujipatia fedha kutokana na uuzaji wa chakula.


Naye, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Zipora Liana amemuahidi Waziri Jafo kwamba stendi hiyo itakuwa ya mfano barani Afrika kwani itajengwa kisasa zaidi.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI JAFO:SITAKI UKANJANJA KATIKA UJENZI WA STENDI YA MABASI MBEZI LUIS
WAZIRI JAFO:SITAKI UKANJANJA KATIKA UJENZI WA STENDI YA MABASI MBEZI LUIS
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgGxVLwgvtnPX4SI3kGzD-SkRNh292DexzYC9odPfJvdcyEF6qKFV-PzDe_N07o9FbjD_pfDsfcOHP4pko_NynHDM2agT8gpctt1AUjige-EcXAMXvRigiyeNtVkAL4U19QJQg8VVHZZys/s640/IMG-20180507-WA0089.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgGxVLwgvtnPX4SI3kGzD-SkRNh292DexzYC9odPfJvdcyEF6qKFV-PzDe_N07o9FbjD_pfDsfcOHP4pko_NynHDM2agT8gpctt1AUjige-EcXAMXvRigiyeNtVkAL4U19QJQg8VVHZZys/s72-c/IMG-20180507-WA0089.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-jafositaki-ukanjanja-katika.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-jafositaki-ukanjanja-katika.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy