TAARIFA KUHUSU WATANZANIA WALIOPATA MATATIZO NCHINI MSUMBIJI
HomeJamii

TAARIFA KUHUSU WATANZANIA WALIOPATA MATATIZO NCHINI MSUMBIJI

  JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI                     TAARIFA KWA VYO...

MHE WAZIRI MKUU AAGIZA KUSIMAMIWA KWA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA NCHI ZENYE LA KUMLINDA MTOTO WA KIKE
MAONESHO YA SABASABA 2017; BABA AMSAJILI MWANAE WA MIAKA 18 NA MPANGO WA "WOTE SCHEME" WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF
MHE:WAZIRI MKUU NI MARUFUKU KUSAFIRISHA MAHINDI NJE YA NCHI BILA KIBALI


 

JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA
MASHARIKI




               
   

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa kuhusu Watanzania waliopata matatizo nchini Msumbiji

Tumepokea taarifa za kukamatwa na kufukuzwa kwa raia wa Tanzania waliokuwa wakiishi katika mji wa Monte Puez ulio Cabo Delgado, Jamhuri ya Msumbiji.

Serikali ya Msumbiji imekiri kuwepo kwa operesheni maalum ya kuwakamata na kuwarudisha raia wa nchi za kigeni wanaoishi katika mji huo bila kufuata Sheria za Uhamiaji za nchi hiyo. Aidha, Serikali hiyo imetaarifu kwamba, zoezi hilo limeanzia mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.

Kufuatia hali hiyo, Ubalozi weti nchini Msumbiji upo eneo la tukio ili kufuatilia suala hili na kujionea hali halisi. Aidha, unaendelea kufanya mawasiliano ya Kidiplomasia na Serikali ya Msumbiji ili kuhakikisha usalama wa Watanzania na mali zao. Inakadiriwa kuwa, Watanzania wapatao elfu tatu (3,000) wanaishi na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika mji huo wa Monte Puez.

Kuanzia zoezi hilo lilipoanza, Raia wa Tanzania wapatao 132 wamesharudishwa nchini. Tarehe 11/02/2017 walirejeshwa raia 58. Tarehe 14/02/2017 wamerejeshwa raia 24 na leo tarehe 15/02/2017 wamesharejeshwa raia 50.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawahakikishia Watanzania kuwa uhusiano kati ya Tanzania na jirani yetu Msumbiji ni mzuri. Hivi karibuni mwezi wa Desemba 2016, Tanzania na Msumbiji zilifanya mkutano wa ujirani mwema uliolenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Mkutano huo uliofanyika kwenye mji wa Pemba ulio Cabo Delgado uliainisha maeneo ya ushirikiano yakiwemo masuala ya biashara na uhamiaji.

Serikali inaendelea kuwakumbusha Watanzania wote waishio ughaibuni, kufuata Sheria na taratibu za nchi hizo wanazoishi.



Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
DAR ES SALAAM. 15 Februari, 2017.

 

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAARIFA KUHUSU WATANZANIA WALIOPATA MATATIZO NCHINI MSUMBIJI
TAARIFA KUHUSU WATANZANIA WALIOPATA MATATIZO NCHINI MSUMBIJI
https://docs.google.com/drawings/u/0/d/s72FFL1YOwo4E2FWB7tK8cA/image?w=665&h=47&rev=1&ac=1
https://lh3.googleusercontent.com/w9YNDPTn4_Iq1w0YKySJXTOVAVNypztFH_UzE2lJiVKsG-DFN7vEFtfbOEWPZO4dyVa5cZIdldwCA-pviMEWdmcG05YuLPwChDb88u2itO1B6jM3g3T8l3i85-hyp6kquT3k7rCBlTDml0nSqA=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/taarifa-kuhusu-watanzania-waliopata.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/taarifa-kuhusu-watanzania-waliopata.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy