WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ameitunuku nishani ya uzalendo kampuni ya Globa...
WAZIRI
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako
ameitunuku nishani ya uzalendo kampuni ya Global Education Link (GEL)
kutokana na mchango inaotoa katika maendeleo ya elimu nchini.
Nishani
hiyo aliitoa leo wakati akizindua mkutano mkuu wa 11 wa Umoja wa Wakuu
wa Shule za Sekondari nchini (TAHOSSA) mkoani Dodoma.
Mkurugenzi
wa Global Education Link (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Rais
wa Wakuu wa Sekondari Tanzania (TAHOSSA), Bonus Ndimbo alisema GEL
imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo katika elimu, sio tu kwa TAHOSSA
hata kwa nchi kwa ujumla.
“Tunaipongeza
sana Global Education Link, kwani imekuwa karibu na jamii, imekuwa
karibu na sekta ya Elimu na maendeleo ya nchi kwa ujumla,” alisema
Katibu Mkuu wa TAHOSSA Diana Matemu.Global Education Link ni kampuni
iliyoanzishwa Mwaka 2006 kwa lengo la kuwaunganisha wanafunzi wa
Tanzania wanaotaka kusoma vyuo vikuu vya nje.
Tangu
imeanza shughuli zake kwa miaka 10 sasa, zaidi ya wanafunzi 5400
wamefaidika kwa kuunganishwa na vyuo mbalimbali vilivyoko Marekani,
Canada, Uingereza, Afrika Kusini, Ukraine, India, Urusi, Malaysia, China
na nyinginezo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza na
Wakuu wa Sekondari Tanzania baada ya kupewa nafasi ya kipekee ya
kuwawakilisha wadau mbalimbali wa elimu waliokaribishwa katika mkutano
huo mbele ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Ufundi stadi Prof Joyce
Ndalichako.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania
(TAHOSSA) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik
Mollel (hayuko pichani).
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa nishani hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Global Education
Link (GEL), Abdulmalik Mollel alishukuru na kusema anafanya hivyo kwa
lengo la kusaidia Serikali na Watanzania kwa ujumla katika kuharakisha
maendeleo nchini.
Kikubwa
ambacho Mkurugenzi wa GEL alisema ni kuwa mpango wa mafunzo kwa
wanafunzi utasaidia kuwafanya wanafunzi kuchagua kozi ambazo zitakuwa na
tija kwao na taifa kwa ujumla.
COMMENTS