MAMLAKA YA UENDELEZAJI KANDA MAALUM ZA KIUCHUMI (EPZA) NA KIWANDA CHA TOOKU VYATOZWA MILIONI 30 KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA
HomeJamii

MAMLAKA YA UENDELEZAJI KANDA MAALUM ZA KIUCHUMI (EPZA) NA KIWANDA CHA TOOKU VYATOZWA MILIONI 30 KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

MAMLAKA ya Uendelezaji Kanda Maalum za Kiuchumi (EPZA)na Kiwanda kilichopo ndani ya Mamlaka hiyo ya Tooku kinachojishughulisha na u...

DKT. SHEIN AWAONGOZA VIONGOZI MBALIMBALI KATIKA HITMA YA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR MZEE ABEID KARUME MJINI UNGUJA
TRA INAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KATIKA KUMBUKUMBU YA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR MHE. SHEIKH ABEID AMANI KARUME
TANESCO YAKABIDHI MRADI WA UMEME KWENYE SHULE YA MSINGI GARAGAZA HUKO KIBAHA



MAMLAKA ya Uendelezaji Kanda Maalum za Kiuchumi (EPZA)na Kiwanda kilichopo ndani ya Mamlaka hiyo ya Tooku kinachojishughulisha na utengenezaji wa nguo zimetozwa faini ya kiasi cha sh.mill 30 kwa kosa la kutililisha maji machafu katika makazi ya watu. 
Ambapo EPZA inapaswa kulipa faini ya Mill20 huku Kampuni ya TOOKU kulipa faini ya milioni 10 na kuhakikisha zinarekebisha mifumo yake ya kupitisha maji taka ipasavyo na kuunganisha katika Mfumo maalum wa Dawasco . 
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano,Luhaga Mpina wakati wa ziara yake ya kukagua baadhi ya viwanda nchini,kuangalia hali ya mazingira ambapo aliambatana na Maofisa mbalimbali kutoka 
Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC), alisema faini hizo zinapaswa kulipwa ndani ya siku 14.Mpina alisema anahasira zaidi na taasisi za serikali zisizofata sheria ya mazingira na kutililisha maji machafu katika makazi ya watu. 
"Nina hasira na taasisi hizi za serikali kwani serikali yenyewe haiwezi kugeuka kupeleka sumu kwa wananchi wake, ambao muda wote inawazuia na kuwakinga wananchi hao hao wasipatwe na 
madhara,"alisema 
Alisema wanapokuta na taasisi ya serikali zinazokiuka miiko iliyoweka katika utunzwaji wa mazingira ni lazma wawapige faini kubwa zaidi kuliko taasisi binafsi ili kuweza kuwa mfano mkubwa kwa jamii.Mpina alisema Mamlaka hiyo ya Uendelezaji Kanda Maalum za Kiuchumi EAPZ ilisema kuwa mfumo wao wa kuyabeba maji taka na kuyapeleka katika mfumo rasmi wa maji taka wa Dawasco umeharibika lakini hawakuweza kuwaandikia NEMC barua ya taarifa juu ya matatizo hayo. 
"Nawataka EPZA ndani ya siku saba mfumo wa kupitishia maji taka wa EPZA uwe umetengenezwa na kukamilika hivyo kuzuia maji taka yanayotoka kutotoka tena kwa sababu yatakuwa yanaingia rasmi katika mfumo wa Dawasco,"alisema.Aidha alisema kwa upande wa Kampuni ya TOOKU yenye inatakiwa kufanya marekebisho makubwa katika mitambo yake ya kutibu maji taka kwani inaonekana kuwa na kasoro. 
"Sheria ya mazingira inakataza utililishaji huu wa maji taka katika mazingira kwani maji yanayotililishwa yanakuwa na kemikali mbalimbali ambazo zinadhuru wanyama,mimea na maisha ya binadamu,kwahiyo viwanda vyetu nchini hatuviruhusu kutililisha maji taka nje kwenda kwenye mazingira na endapo yatatililishwa yanapaswa kupimwa,kuhakikiwa na kudhibitishwa kuwa hayana madhara,"alisema . 
Aidha alisema katika ukaguzi walioufanya mamlaka hiyo na kiwanda hicho hakikuweza kuonyeshwa ubora wa maji yanayotililika kuja katika mazingira ya watu kwani maji yanayotililika kutoka katika Mamlaka hiyo na Kiwanda hicho cha yanatoka na rangi. 

Kwa Upande wake Mratibu wa Kanda ya Mashariki NEMC , Jafari Chimgege alisema katika kiwanda cha Tooku kimekuwa mbaya wa kutibu maji taka na kusababisha kumwaga maji machafu katika mazingira bila kuyatibu ambapo ni kinyume cha sheria. 
"Viwanda vinafahamu kuwa vinapomwaga maji machafu katika mazingira bila kuyatibu au kuyapeleka katika mifumo rasmi ni kosa,kiwanda hiki cha TOOKU na Mamlaka hii ya EAPZ vimefanya kosa,"amesema.Chimgege amesema maji yanayotilishwa na viwanda mbalimbali 
katika mito ni makosa kwani maji hayo yanakuwa na madhara kwa wananchi. 
Nae Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Muongozo,James Ngoitanile alisema wananchi wake wamekuwa wakipata shida na maji hayo wakati mwingine yanawaletea madhara.Amesema wapo watu wanaolima michicha ambao wanatumia maji ya mto huo kumwagilia hivyo yanavyochanganyika na maji hayo yanasababisha watu kula mbogamboga zenye kemikali.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Mazingira katika kituo cha uwekezaji cha EPZA, kilichopo Ubungo Jijini Dar es Salaam. 
 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia shughuli za uzalishaji wa nguo katika kituo cha uwekezaji cha EPZA mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kituo hicho kilichopo Ubungo Jijini Dar es Salaam. 
 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia suruali aina ya Jinsi zinazozalishwa katika kituo cha uwekezaji cha EPZA wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mazingira mapema hii leo Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia mfereji wa maji machafu yanayotiririshwa na kituo hicho ambayo yamekuwa ni kero kwa wananchi.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAMLAKA YA UENDELEZAJI KANDA MAALUM ZA KIUCHUMI (EPZA) NA KIWANDA CHA TOOKU VYATOZWA MILIONI 30 KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA
MAMLAKA YA UENDELEZAJI KANDA MAALUM ZA KIUCHUMI (EPZA) NA KIWANDA CHA TOOKU VYATOZWA MILIONI 30 KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgefK25bfXz5vswPWE69k30syqCFXoaHLOoLEW5gYrP7WOHGKPQ0E4Z4t0TzLg7kwBJWvYSgoDdoaGPC7uRgyJfQrGiOOzopTzGNHQ7QIG3rXKlp9oQn8CY0GMgmRhqPLSmD2v6anEAbUU/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgefK25bfXz5vswPWE69k30syqCFXoaHLOoLEW5gYrP7WOHGKPQ0E4Z4t0TzLg7kwBJWvYSgoDdoaGPC7uRgyJfQrGiOOzopTzGNHQ7QIG3rXKlp9oQn8CY0GMgmRhqPLSmD2v6anEAbUU/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/mamlaka-ya-uendelezaji-kanda-maalum-za.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/mamlaka-ya-uendelezaji-kanda-maalum-za.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy