Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa na Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Kamishna Juma Malew...
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa na Kaimu Kamishna Mkuu wa
Magereza Kamishna Juma Malewa wakizungumza na waandishi wa Habari leo
katika gereza la Ukonga Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na
Mratibu wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza Bw. Julious Chege katika
gereza hilo la Ukonga, jijini Dar.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na
Kaimu kamishna wa Jeshi la Magereza Juma Malewa,mara baada ya kukagua
Kiwanda cha kutengeneza Samani Katika gereza la Ukonga.
Na Anthony John Glob Jamii.
NAIBU Waziri Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelitaka jeshi la zimamoto na Uhamiaji kutoshona sare zao za uraiani, badala yake wakashone katika jeshi la Magereza ili kubana matumizi ya serikali.
Masauni ameyasema hayo leo katika ziara yake ya kutembelea Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam, ambapo amekagua Kiwanda cha Magereza kinachojishughulisha na ushonaji wa nguo za wafungwa na nguo za askari Magereza.
Sanjari na hayo Mhandisi Masauni ametoa wito kwa Watanzania kwa kununua bidhaa mbali mbali zinazo tengenezwa na jesi la Magereza ili kuunga mkono kwa kazi nzuri wanazozifanya.
Aidha amewapongeza askari wa jeshi la Magereza kwa kujitolea kujenga nyumba zao bila kusubiri serikali kuwajengea na kuwaahidi kuwa Serikali itaandaa bajeti Mwakani ili kumalizia maeneo machache yaliyo baki.
Naye Kaimu Mkuu wa Magereza Kamishina Msaidizi. Juma Malewa amesema Jeshi hilo linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi kama mashine za kushonea nguo, na mashine za za ufundi selemala, ukosefu wa mtaji wa kuendesha shughuli za kilimo, hivyo amesema pindi serikali itakapo wawezesha watajitosheleza kwa chakula na mahitaji mengine.

COMMENTS