Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mk...
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.
Aziz Mlima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume ya Pamoja
ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Kenya uliofanyika
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili maeneo mbalimbali ya
ushirikiano ikiwemo sekta ya Elimu, Afya na Kilimo.
Balozi
wa Kenya hapa nchini, Mhe. Chirau Ali Mwakwere akifuatilia ufunguzi wa
Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na
Kenya
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi. Talha Mohammed (kulia) naye akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa JPC.
Balozi Ben Ogutu, Kiongozi wa Ujumbe wa Kenya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Kenya.
Mkurugenzi
wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akizungumza wakati wa Mkutano
wa JPC kati ya Tanzania na Kenya.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia alikuwa mshereheshaji
akizungumza, Mindi Kasiga.
Sehemu ya wajumbe kutoka Kenya wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa JPC.
Sehemu ya wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano
COMMENTS