Na Evelyn Mkokoi - Bagamoyo SERIKALI imeiagiza Baraza la hifadhi ya Mazingira (NEMC ) na Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa R...
Na
Evelyn Mkokoi - Bagamoyo
SERIKALI
imeiagiza Baraza la hifadhi ya Mazingira (NEMC ) na Idara ya
Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais
kufanya tathimini ya awali ya kuangalia ni namna gani itaweza kuzuia maji
ya bahari kuingia katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
na kuharibu miundombinu yake ambapo hadi sasa takribani mita
70 hadi 100 ya bahari imeisogelea taasisi hiyo.
Akizungumza jana wilayani Bagamoyo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Luhaga Mpina wakati wa ziara ya kutembelea Taasisi hiyo na kujionea ni namna gani bahari inavyosogea katika taasisi hiyo na kuanza kuathiri baadhi ya majengo.
Alisema kutokana na hali hiyo kuwa ya dharura ameziagiza mamlaka hizo kufanya tathimini ya awali
ambapo kufikia Januari 30 mwakani watapaswa kukabidhi ripoti ya awali kwa serikali na kujua nini
kifanyike katika kunusuru taasisi hiyo na kuifanya mahala pazuri pa kujifunzia masuala ya utamaduni.
Mpina alisema ripoti hiyo itaweza kupelekwa serikalini ili mipango madhubuti ianze kufanyika ya
kuhakikisha taasisi hiyo inakuwepo na inaendelea kutoa mafunzo yake kama kawaida bila kuathiriwa
na usogelewaji wa bahari katika maeneo hayo.
"Januari 30 mwakani tutapata hiyo ripoti na kuipeleka serikalini na kuangalia ni namna gani
tutakavyonusuru taasisi hiyo na kama kutahitajika utafiti mwingine wa kina kuhusiana na jambo hili
utaweza kufanyika na kujua nini kifanyike katika maeneo haya kama kutengeneza Makinga maji au
Ukuta,"alisema Mpina
Alisema hali ya bahari kuhamia katika maeneo ya nchi kavu inatokana na kuwepo kwa mabadiliko ya
tabia nchi yanayotokea baharini ambapo kwa sasa kina cha bahari kimeweza kuongezeka kufikia
Sentimita 19 na kusababisha madhara ya maji kusogea katika maeneo ya nchi kavu.
Mpina alisema takribani majengo matatu ya taasisi hiyo yapo hatarini kuathirika ambayo yanajumla
ya thamani ya kiasi cha sh. Bilioni 1.6 ambapo yatasababisha hasara kubwa kwa majengo pamoja na
taasisi hiyo.
Aidha mpaka sasa kuna baadhi ya fukwe tayari zimeanza kufanyiwa utaratibu wa kujengwa kwa
kingo zikiwemo fukwe za Pangani Tanga, Kilimani Zanzibar, Kisiwa Panza Pemba, pamoja na fukwe za
Ocean road Dar es Salaam.
Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Dkt. Herbert Makoye
alisema taasisi yao inatatizo kubwa ya kusogelewa na bahari na kusababisha athari kubwa katika
baadhi ya madarasa.
Alisema kwa sasa bahari inazidi kusogelea chuo hali inayotishia uwepo wa chuo hicho endapo jitihada
dhabiti hazitaweza kuchukuliwa kwani hadi sasa uoto wa asili umeanza kutoweka kidogo kidogo.

Wakati huohuo,
Kufuatia malalamiko ya wakazi wa kata ya Bunju, Naibu Waziri Mpina
alitembelea maeneo hayo yanayoathiriwa kwa kiasi kikubwa na maji ya mvua, na
kuharibu miundombinu na mazingira na kupelekea afya za wakazi wa maeneo hayo
kuwa hatarini kuathiriwa na magonjwa, Hali ambayo ilimlazimu Mpina kutoa agizo
kwa NEMC, Idra ya Mazingira Ofisi ya Makmu wa Rais na Manispaa ya Kinondoni kufanya
Tathnini ya mazingira katika eneo hilo na kuja na mpango mkakati wa muda mfupi
na mrefu ili kuweza kunusuru hali hiyo.
Mpina aliwaasa wakazi wa eneo hilo pia kuzingatia
ujenzi wa mipango miji na kuacha njia za maji na maeneo oevu.
Katika Picha Eneo la Fukwe ya Bagamoyo upande wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni linavyotishiwa kuharibika vibaya kutokana na athari za mabadiliko ya Tabianchi. |
Dkt Herbert Makoye Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni ya Bagamoyo akiongea na vyombo vya
habari kuhusu uhabifu wa fukwe utokanao na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
|
COMMENTS