HomeJamii

WAZIRI MKUU AZINDUA MAABARA YA KUPIMA MADINI

*Ni ya kwanza Afrika, inauwezo wa kutambua aina za madini na yalikotoka WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua maabara ya kisasa y...

MAZISHI YA SIR GEORGE KAHAMA KUFANYIKA KESHO, SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA ATOA POLE KWA WAFIWA
RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU YA CHAMWINO, DODOMA, LEO
DKT. SHEIN AKUTANA NA MKUU WA MAJESHI JENERALI VENANCE MABEYO IKULU YA ZANZIBAR


*Ni ya kwanza Afrika, inauwezo wa kutambua aina za madini na yalikotoka

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua maabara ya kisasa ya na ya kwanza barani Afrika yenye uwezo wa kupima na kutambua aina mbalimbali za madini.

Amesema maabara hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya umiliki wa madini na kudhibiti utoroshwaji wa madini mbalimbali kati ya nchi moja na nyingine.

Maabara hiyo imefunguliwa leo (Ijumaa, Juni 8, 2018) katika Kituo cha Madini na Jiosayansi  cha Afrika  (AMGC) kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema uzinduzi wa maabara hiyo utawezesha wataalamu kutambua aina za madini na nchi yanakotoka, hivyo kuondoa migogoro ya umiliki wake. 

“Maabara hii litatuweza kulinda madini yetu na kufanya biashara ya madini vizuri. Pia hii ni fursa nzuri kwa nchi za Afrika kutumia maabara hii kupima madini yao na kubaini yalikotoka,” amesema.

Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wa kituo hicho kuhakikisha wanaziwesha nchi wanachama kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya madini pindi zinapohitaji.

Pia Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara hiyo pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalamu watakaoiendesha.

Waziri Mkuu, pia ameiomba Serikali hiyo kutoa mafunzo hayo kwa Watanzania wengi zaidi ili kuongeza idadi ya wataalamu wa kuendesha maabara hiyo.

Pia, Waziri Mkuu amefungua Mkutano 38 wa Mawaziri wa Madini kutoka nchi Wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika katika kituo cha AMGC.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini ikiwa ni pamoja na Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama zilizosheheni wanyama wa aina mbalimbali pamoja na fukwe za bahari.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JUNI 8, 2018.



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AZINDUA MAABARA YA KUPIMA MADINI
WAZIRI MKUU AZINDUA MAABARA YA KUPIMA MADINI
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/waziri-mkuu-azindua-maabara-ya-kupima.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/waziri-mkuu-azindua-maabara-ya-kupima.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy