MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA YA SIKU 5 MKOANI MWANZA
HomeMikoani

MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA YA SIKU 5 MKOANI MWANZA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Nyamagana kabla ya kuweka ji...

UMOJA WA MATAIFA YAIMWAGIA SIFA JWTZ NA SERIKALI YA JPM
MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI KOROGWE
UONGOZI WA MKOA RUKWA WACHANGIA MILIONI 5.7 KUMALIZIA UJENZI WA MSIKITI SUMBAWANGA







 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Nyamagana kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa machinjio ya Nyakato.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya ujenzi  wa machinjio ya Nyamagana kutoka kwa Mhandisi wa jiji la Mwanza Ndugu Ezekiel Kunyalanyala (kushoto) kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa machinjio ya Nyakato.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Jengo la Utawala Manispaa ya Ilemela.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikikabidhi madawati kwa Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ambayo
yalitolewa na Ofisi ya Bunge ambapo zaidi ya madawati 1074 yalikabidhiwa kwa wilaya ya Nyamagana na Ilemela.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kufungua jengo la Manispaa ya Ilemela. 

                                   .............................................................................................. 



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muda wa mwezi Mwezi Moja kuanzia leo tarehe 18-Nov-2016 kwa watendaji na viongozi waandamizi wa wilaya ya Ilemela wahamie kwenye wilaya hiyo haraka iwezekanavyo na waache tabia ya kukaa kwenye wilaya nyingine kwa kisingizio cha kukosa nyumba za serikali.



Makamu wa Rais ametoa agizo hilo katika hotuba yake kwa wananachi na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi jengo
la utawala la Manispaa hiyo na kukabidhi madawati 1,074 yaliyotolewa na ofisi
ya Bunge.



Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na tabia hiyo na amewataka viongozi
hao wahamie karibu na maeneo yao ya kazi kabla ya muda aliotoa kwisha ili waweze kuwa karibu na wananchi katika kuwasaidia kutatua kero na matatizo yanayowakabili
kwa haraka.




Akiwa katika wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wakati anaweka jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati wa mchinjio ya Nyakato jijini Mwanza, Makamu wa Rais ameuagiza uongozi jiji la Mwanza kusimamia kikamilifu mradi wa ukarabati wa machinjio  ya Nyakato na watendaji
watakaobainika kuhujumu mradi ambao utagharimu zaidi ya shilingi bilioni Tatu wachukuliwe hatua kali za kisheria.



Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwa wananchi na watendaji wa jiji la Mwanza waliohudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati wa
machinjio ya Nyakato unaohusisha uboreshaji wa jengo la machinjio, tanki la kuhifadhi maji,ujenzi wa vyumba vya baridi vya kuhifadhi nyama na ujenzi wa mtambo wa kutibu majitaka yanayotoka kwenye machinjio hiyo.




Makamu wa Rais katika hotuba yake, amesema hategemei hata kidogo ukarabati wa machinjio hiyo ufanyike chini ya kiwango kwa sababu ni mradi wa kibiashara ambao ukikamilika na kuanza kufanya kazi utasaidia jiji la Mwanza kupata mapato yatakayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.



Makamu wa Rais pia amemwagiza Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ahakikishe anasimamia
uundaji wa menejimenti ya machinjio hiyo ambayo itafanya kazi vizuri na sio kuingiza watu ambao hawana uwezo ambao watakwamisha utendaji kazi wa machinjio
hiyo.




Kuhusu ukusanyaji wa kodi, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza watendaji wa Halmashauri zote za mkoa wa Mwanza waongeze kasi ya ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa njia ya kielekroniki kutoka kwenye vyanzo mbalimbali fedha ambazo zitasaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi mkoani humo.



Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wananchi nchini wahakikishe wanadai risiti
wanaponunua bidhaa mbalimbali kwani kufanya hiyo watasaidia kuongeza mapato
yake ambao yataelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.




Katika Mkutano wake wa Majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya Siku Tano mkoani Mwanza na viongozi wa mkoa wa Mwanza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewasisitiza viongozi na watendaji wa mkoa wa Mwanza wafanye kazi kwa bidii katika
kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za umma.



Ameonya kuwa serikali ya awamu ya Tano haitasika kuwachukulia hatua kali viongozi na watendaji ambao watakwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma kwenye maeneo yao ya
kazi.



Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa mkoa wa Mwanza kusimamia kikamilifu katika kulinda hali ya amani na Utulivu na wachukue hatua  kali kwa watu wanaotaka kuharibu  amani ya nchi.



Makamu wa Rais amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku Tano mkoani Mwanza kwa kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya mbalimbali ya
maendeleo katika wilaya za Ilemela,Misungwi, Kwimba, Magu na Nyamagana.




BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA YA SIKU 5 MKOANI MWANZA
MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA YA SIKU 5 MKOANI MWANZA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihm1dsWwEsFk1KvfoWIjSu4PMIrM-VdQ4HlZSw43QB6FIH29xJoiBoQ-3l1dGZcwuFSQ36reh2UMMNQSYZ_D0nhS_nN2VgNtrP__-ik7EhXp5fD4CoRIHlVWGJJXPv7EESJT3V6Klo3Bs/s640/6.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihm1dsWwEsFk1KvfoWIjSu4PMIrM-VdQ4HlZSw43QB6FIH29xJoiBoQ-3l1dGZcwuFSQ36reh2UMMNQSYZ_D0nhS_nN2VgNtrP__-ik7EhXp5fD4CoRIHlVWGJJXPv7EESJT3V6Klo3Bs/s72-c/6.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/makamu-wa-rais-amaliza-ziara-ya-siku-5.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/makamu-wa-rais-amaliza-ziara-ya-siku-5.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy