MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA MAGOMENI KOTA
HomeJamii

MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA MAGOMENI KOTA

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin...

KAMPUNI YA TOOKU GARMENT YATOA MSAADA VIFAA VYA TEHEMA KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
MRADI WA ORIO MUARUBAINI WA TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI
MEYA MWITA AUNGANA NA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUPIMA MAGONJWA YA KISUKARI NA SHINIKIZO LA DAMU









  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma  kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma  kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo Novemba 18, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally  Happy.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokagua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam Novemba 18, 2016.  Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happy. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajenzi wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam kukagua mendeleo ya mradi huo Novemba 18, 2016. 
ENDELEENI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI - MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Waislamu nchini waendelee kushirikiana na Serikali kulinda na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

Aidha, amewasihi waislam kuimarisha umoja ,upendo ,mshimano miongoni mwao kwa kushirikiana na jamii zinazowazunguka bila kujali tofauti zao za kiimani. 

Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Novemba 18, 2016) wakati akishiriki sala ya Ijumaa katika msikiti wa Kichangani, Magomeni jijini Dar es Salaam. 

Amesema uwepo wa dini umewezesha nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu hivyo kila mmoja ahakikishe suala hilo linaendelezwa.

Pia amewashauri waumini na viongozi wa dini kuzingatia maadili ya dini ili kuepusha migongano isiyo ya lazima hasa taasisi zinapokuwa na miradi. 

Waziri Mkuu alitolea mfano msikiti huo wa Kichangani chini ya Sheikh  Walid umeweza kusuluhisha hitilafu wenyewe bila kukimbilia Serikalini au mahakamani kusuluhishwa.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Waislamu wana jukumu la kuwafunza elimu ya dini watoto wao na kuhakikisha wanakua kwenye imani na kujengeka katika maadili mema.

Amesema dini inajenga maadili mema kwa mtoto na kumwezesha kukua katika misingi ya uvumilivu na inamuwezesha kumtambua Mwenyezi Mungu. 

“Nimefarijika kuona vijana wengi wameshiriki katika sala hii ya Ijumaa. Nawaomba wazazi waendelee kuelimisha watoto umuhimu wa kufanya ibada,” amesema.

“Tuendelee kuwafundisha vijana wetu umuhimu wa kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kidini ili wakikua waweze kuiendeleza kwa vizazi vijavyo,” amesema.

Waziri Mkuu amewaomba waumini hao waendelee kuwaombea viongozi wa kitaifa ili waweze kutekeleza vizuri majukumu yao na kufikia malengo yanayotarajiwa na wananchi. 


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
IJUMAA, NOVEMBA 18, 2016.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA MAGOMENI KOTA
MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA MAGOMENI KOTA
https://i.ytimg.com/vi/hkZd8nrOICA/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/hkZd8nrOICA/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/majaliwa-atembelea-mradi-wa-ujenzi-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/majaliwa-atembelea-mradi-wa-ujenzi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy