WAKAZI WA UKEREWE MWANZA WATAKIWA KUITUMIA MELI MPYA NA YA KISASA, MV NYEHUNGE II.

Mwonekano wa Mv Nyehunge kwa ndani, sehemu ya abiria kukaa. Na George Binagi-GB Pazzo @BMG Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mong...









Mwonekano wa Mv Nyehunge kwa ndani, sehemu ya abiria kukaa.

Na George Binagi-GB Pazzo @BMG

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, mwishoni mwa wiki amefanya uzinduzi wa Meli Mpya ya Mv Nyehunge ya pili (II) inayofanya safari zake kati ya Mwanza na Ukerewe na kuwataka wakazi wa Ukerewe kuitumia fursa hiyo kujiinua kiuchumi.



Mongella alisema Meli hiyo itasaidia kuondokana na adha ya usafiri kwa wakazi wa Visiwa vya Ukerewe kwa kuwa imeongeza idadi ya Meli zinazofanya safari kati ya Jiji la Mwanza na visiwa hivyo.



Aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kusafirisha bidhaa zao kati ya Ukerewe na Jiji la Mwanza ili kujiinua kiuchumi huku akisisitiza Kampuni ya Nyehunge inayomiliki Meli hiyo kuzingatia vigezo vya usalama katika uendeshaji wa safari zake.



Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyehunge, Said Mohame, alisema Meli hiyo inaongeza safari kati ya Visiwa vya Ukerewe na Jiji la Mwanza na kufikia safari tatu kwa siku huku suala la nauli nafuu likizingatiwa ili kuondoa changamoto ya usafiri waliyokuwa nayo wakazi wa Ukerewe. Nauli za Ukerewe katika Meli hiyo ni Shilingi 6,000 kwa 7,000.



Baadhi ya wasafiri wa Ukerewe walipongeza ujio wa Meli ya Mv Nyehunge ambapo wamebainisha kwamba itawasaidia kusafirisha kwa wakati bidhaa na mazao ya chakula kati ya Ukerewe na Jiji la Mwanza.



Meli hiyo ya Mv Nyehunge II ina uwezo wa kubeba abiria 500, magari madogo 40 na tani 284 za mizigo ambapo imejengwa na kampuni ya wazawa ya Songoro Marine Transport ya Jijini Mwanza kwa zaidi ya shilingi Milioni 800.



Tazama HAPA Uzinduzi Ulivyokuwa

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAKAZI WA UKEREWE MWANZA WATAKIWA KUITUMIA MELI MPYA NA YA KISASA, MV NYEHUNGE II.
WAKAZI WA UKEREWE MWANZA WATAKIWA KUITUMIA MELI MPYA NA YA KISASA, MV NYEHUNGE II.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEibsR6mB9PN5s1DbzWewb8gQL1XEtwlkGcZyec4Lp4Z2KsCPEjprkZgvW_061zdbF0IqqxnQkAQkEbQoHEt8lY9QgI6HXcdfi4ALm54n4MVshxqiBS8_sO9xdXi9MrVcpbEhMQtENTkByc/s640/11.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEibsR6mB9PN5s1DbzWewb8gQL1XEtwlkGcZyec4Lp4Z2KsCPEjprkZgvW_061zdbF0IqqxnQkAQkEbQoHEt8lY9QgI6HXcdfi4ALm54n4MVshxqiBS8_sO9xdXi9MrVcpbEhMQtENTkByc/s72-c/11.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/10/wakazi-wa-ukerewe-mwanza-watakiwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/wakazi-wa-ukerewe-mwanza-watakiwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy