WANANCHI WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM
HomeJamii

WANANCHI WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

Na Dotto Mwaibale WANANCHI wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam wamempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo, Kisare Matiku Makori kwa kuwe...

MEYA WA JIJI AFANYA ZIARA SOKO LA KARIAKOO, ABAINI WIZI WA FEDHA KATIKA VIZIMBA VYA SOKO HILO
TAASISI YA MO DEWJI YATOA ZAWADI KITUO CHA TUMAINI LA MAISHA
WATU 9 WAKAMATWA KWA UDUKUZI WA TOVUTI ZA SERIKALI




Na Dotto Mwaibale


WANANCHI wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam wamempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo, Kisare Matiku Makori kwa kuweka utaratibu wa kusikiliza kero zao kwa ajili ya kuzitafutia utatuzi.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti  jijini Dar es Salaam jana walisema utaratibu anaoufanya mkuu huyo wa wilaya unapaswa kuigwa na viongozi wengine kwani unakwenda na kasi ya kazi ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli ya hapa kazi tu.




"Binafsi nampongeza mkuu wetu wa wilaya kwa kazi hiyo anayoifanya ya kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi wake na kuzitafutia utatuzi ni jambo zuri na hasa anapokuwa na wasaidizi wake, wanasheria na Katibu Tawala " alisema Fabiola Sumary mkazi wa Mbezi kwa Yusuph.


Sumary alisema anapowashirikisha wenzake hasa wataalamu wake wakati wa kusikiliza kero hizo inasaidia kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja bila ya kupoteza muda mwingi.



Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la mama Mshindo alisema mpango huo umesaidia kwa namna moja au nyingine kupunguza msongamano ofisi ya mkuu wa mkoa ambako wananchi wengi walikuwa wakikimbilia kupeleka malalamiko yao.


Mkazi mwingine Francis Malota alisema mkuu huyo wa wilaya bila ya kujali jua, mvua  na kula amekuwa akiwasikiliza wananchi wake zaidi ya 70 kila siku jambo linaloonyesha jinsi anavyowajali.


"Tangu asubuhi hadi saa moja usiku amekuwa akisikiliza changamoto mbalimbali za wananchi wake tunamuombea kwa mungu amzidishie hekima hiyo" alisema Caroline Mwangoka mkazi wa Mbezi kwa Mangi.


Mkuu huyo wa wilaya kila wiki amejiwekea utaratibu wa kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi wake ikiwemo migogoro ya ardhi, jamii na ndoa.



(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANANCHI WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM
WANANCHI WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCUPM-VLLA9uB2XFx3HcmPDDfMVrXWcIYHdfPH0eYKoZzpW05W7RhcQg2udr_WhXlutFSQwBgPl_JhqtAU0dSrF0FYRKzom8WTCKMfVSEAdqAuLIRGjawiTf9WXNsK_JlkdGvy_rClqXRS/s320/DC%252BKISARE.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCUPM-VLLA9uB2XFx3HcmPDDfMVrXWcIYHdfPH0eYKoZzpW05W7RhcQg2udr_WhXlutFSQwBgPl_JhqtAU0dSrF0FYRKzom8WTCKMfVSEAdqAuLIRGjawiTf9WXNsK_JlkdGvy_rClqXRS/s72-c/DC%252BKISARE.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/wananchi-wampongeza-mkuu-wa-wilaya-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/wananchi-wampongeza-mkuu-wa-wilaya-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy