Wasanii wa Lusaka wakicheza ngoma ya asili ya Zambia katika mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB uliofany...
Wasanii wa Lusaka wakicheza ngoma ya asili ya Zambia katika mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi Zambia Mei 24, 2016. Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. |
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina mpango wa kujenga njia ya
umeme kutoka Mbeya hadi Zambia kupitia Tunduma ili kupunguza tatizo la umeme
linaloikabili nchi hiyo.
“Serikali ya Tanzania inajenga njia ya umeme ya msongo wa KV 400 kutoka
Iringa - Dodoma – Singida – Shinyanga ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme
unaolenga kuunganisha Zambia, Tanzania na Kenya,” amesema.
Amesema upembuzi yakinifu kwa ajili KV400 kutoka Iringa hadi Mbeya
umekwishakamilika tangu mwaka 2012, na hivi sasa Serikali inatafuta fedha kwa
ajili kuunganisha kipande cha kutoka Mbeya na gridi ya Taifa ya Zambia.
Waziri Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais,
Dk. John Pombe Magufuli, ametoa ufafanuzi huo leo mchana (Jumanne, Mei 24,
2016) wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wakuu wa nchi na Serikali
uliohusu Nishati na Mabadiliko ya TabiaNchi kwenye ukumbi wa mikutano cha
kimataifa wa Mulungushi.
Amesema ili kukabiliana na changamoto ya nishati barani Afrika, nchi za
bara hili zinahitaji kuwa na fedha ama mitaji, teknolojia ya kisasa na
wataalamu wenye ujuzi wa kutosha jambo ambalo amesema ni gumu kulikamilisha
kila nchi peke yake.
Amesema ili kukaribisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme, Tanzania
inafanyia marekebisho sheria zake ili kuruhusu uwekezaji kwenye sekta hiyo.
Akizungumzia kuhusu hali ya nishati Tanzania, Waziri Mkuu alisema Tanzania
imebarikiwa kuwa na gesi asilia yenye ujazo wa futi trilioni 57.25 (tcf), makaa
ya mawe yenye uhjazo wa tani bilioni 1.9 (asilimia 25 imevumbuliwa), umeme wa
nguvu ya maji wa gigawati 4.7 ambazo ni asilimia 12 tu ndiyo inatumika. Pia
alisema Tanzania ina deposits za urani yenye ujazo wa ratili milioni 200 (200
million pounds), joto la ardhini (geothermal) linaloweza kuzalisha umeme wa
megawati zaidi ya 5,000. “Hivyo ni mbali na vyanzo vya umeme utokanao ua upepo
na jua,” alisema.
Akizungumzia kuhusu usambazaji wa umeme vijijini, Waziri Mkuu alisema
Tanzania kupitia REA imefanikiwa kusambaza umeme kwenye asilimia 52 ya vijiji
vyote na inatarajia kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2025.
Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo
alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli
linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.
“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya
jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,”
alisema.
Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário
Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo
alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli
linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.
“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya
jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,”
alisema.
Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema
masuala ya nishati yanahitaji uwekezaji mkubwa kwa hiyo akashauri makampuni
kuungana kwenye uwekezaji na kuibua miradi ambayo ina tija (feasible and
viable).
Waziri Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu
Kijaji, wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA
WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MEI
24, 2016.
Wasanii
wa Lusaka wakicheza ngoma ya asili ya Zambia katika mkutano wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika - ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha
Mlungushi Zambia Mei 24, 2016. Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Zambia, Edgar Lungu
katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB kwenye Kituo cha
Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos
Agostino do Rosario katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB
kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei
24, 2016.
Rais
wa Zambia, Edgar Lungu akifungua Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika - ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka
Zambia , Mei 24, 2016. Kushoto kwake ni Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo, Rais wa ADB, Akinwumi Adesina (wa tatu kushoto), Rais wa Chad amabaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), IdrissaDeby Itno ((katikati), Rais wa Rwanda, Paul Kagame na viongozi wengine.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika - ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi
kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto
ni Makamu wa Rais wa Nigeria, Prof. Yemi Osinbojo, Rais wa Chad, Idriss
Debyo, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos
Agostino do Rosario (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
COMMENTS