Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Disemba 16, 2014 na Rais wa ...
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo,
Jumanne, Disemba 16, 2014 na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete,
Jaji Werema amesema kuwa ameomba
kujiuzulu kwa sababu ushauri wake
kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta
Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema
kwa utumishi wake ulioongozwa na
uaminifu na uadilifu.
Jaji Frederick Werema akiingia Bungeni katika kikao cha mwisho cha Bunge la Disemba 2014 |
COMMENTS