Bw. Felix Ntibenda, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha NA K-VIS BLOG RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, D...
Bw. Felix Ntibenda, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha |
NA K-VIS BLOG
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya
mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha kuanzia leo Alhamisi, Agosti 18,2016. Taarifa fupi iliyotolewa kwa
vyombo vya habari na ofisi ya Waziri Mkuu mapema leo, imesema, Rais amemteua
aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mrisho Gambo, kuchukua nafasi hiyo na
ataapishwa Ijumaa Agosti 19, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais amemuhamishia ofisi ya Waziri Mkuu ambako
atapangiwa kazi nyingine. Bw. Ntibenda anakuwa Mkuu wa mkoa wa pili
"kufutwa" kazi, baada ya kuteuliwa kushika madaraka hayo chini ya
mwaka mmoja, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anne Kilango Malecela, yeye alikuwa mkuu wa
mkoa wa kwanza kuhudumu kwa muda mfupi kwenye nafasi hiyo, baada ya Rais
kutengua uteuzi wake kwa kutoa taarifa isiyo sahihi juu ya watumishi hewa.
Ingawa
safari hii hakuna sababu yoyote iliyoelezwa kuwa ndiyo iliyopelekea Mkuu wa
Mkoa Ntibenda "kufutwa' kazi, lakini katika siku chache zilizopita,
kumekuwepo na mfululizo wa vitendo vya hujuma za majengo ya
shule za umma mkoani humo ambapo Agosti 6, 2016 mabweni mawili ya wanafunzi wa
shule ya sekondari Longido yaliteketea kwa moto na kufanya shule tatu za
serikali kuchomwa moto ndani ya wiki moja. Hali hiyo ilimfanya hata Mkuu wa
wilaya ya Longido, Daniel Chongolo, kueleza kuwa matukio hayo ni hujuma dhidi
ya shule za umma na kwamba serikali itaanzisha msako wa kuwabaini watu hao
wanaoendesha hujuma ya kuharibu shule za umma. Ni
majuzi tu Bw. Ntibenda akiongozana na kamatiya ulinzi na
usalama ya mkoa huo, aliagiza kukamatwa kwa walimu wote, walinzi wote na
wanafunzi waliohusika na uhalifu huo wa kuchoma moto majengo ya shule.Masanduku ya kuhifadhia vitu, ya wanafunzi yaliyoharibika kufuatia moto kuunguza bweni lao huko Arusha |
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda. akizungumza na wanafunzina walimu wa shule moja mkoani humoambayo bweni al wanafunzi liliteketea kwa moto hivi majuzi |
Bw. Mrisho Gambo, Mkuu mpya wa mkoa wa Arusha
COMMENTS