Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Samani, Shafik Bhatia (kushoto) na Mwenyekiti wa Shirikisho la Woodworking Tanzania (TAWOFE), ...
KAMPUNI ya Furniture
Centre (FCDL), na Shirikisho la Watengenezaji Samani Nchini (TAWOFE), wamesaini
makubaliano (MoU) kuongeza ubora wa bidhaa za samani zinazotengenezwa nchini na
kuzifanya zipate soko ndani na nje ya nchi.
Makubaliano haya
yamekamilika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi ikiwa ni mwendelezo wa Tathimini iliyofanywa na Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya
jirani, katika kuiwezesha sekta ya Samani nchini kupitia vikundi na makampuni
ya ndani.
Tathimini hiyo ya Baraza
ya mwaka 2008, ilijikita katika kubaini mahitaji na changamoto zinazoikabili
sekta ya samani hapa nchini. Baraza liliweza kuandaa warsha iliyohudhuriwa na
wadau mbalimbali na ambapo matokeo ya tathmini hiyo yaliwasilishwa. Wadau
kutoka sekta ya umma na binafsi walishiriki katika mrejesho wa tathmini hiyo na
wao pia kuchangia maoni zaidi kwa ajili ya kuiboresha.
Washirika hao walisaini
makubaliano hayo katika hafla
iliyoshuhudiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na
Uwekezaji), Dk Mary Nagu.
Akizungumza katika
hafla hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,
Dk Anacleti Kashuliza, alisema pamoja na kuwepo kwa fursa kubwa ya soko la
samani hapa nchini bado ushiriki wa vikundi na makampuni ya ndani katika soko
hilo ni mdogo sana kulinganisha na samani zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.
Alisema tunatoa wito
kwa taasisi za Umma na Binafsi ziunge
mkono jitihada hizi kwa kununua samani toka kwa watengenezaji samani wa ndani na ili kuwapa ushirikiano zaidi
utakaowezesha kuimarisha sekta ya samani zitengenezwazo ndani ya nchi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti
wa TAWOFE, Bw Fredrick Waibi, alielezea makubaliano kati ya FCDL na TAWOFE ni
mkakati mzuri utaomjengea uwezo fundi seremala kuweza kutengeneza bidhaa
zitakazoweza kukubalika kimataifa, kuongeza tija kazini na kupunguza umaskini
kati ya mafundi seremala.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa
FCDL, Bw Shafik Bhatia, alisema kama wadau muhimu wa samani nchini wameona
umuhimu na wanajivunia kushirikiana na
Tawofe katika kuboresha huduma za samani nchini .
Katibu Mtendaji wa
Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Dk Anacleti Kashuliza (wa pili kulia) akiweka
saini makubaliano ya ushirikiano kati ya FCDL na TAWOFE katika kuboresha
utengenezaji wa samani nchini. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji
na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu (wa kwanza kulia) anayeshuhudia makubaliano hayo.
COMMENTS