KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA MITA ZA LUKU CHA INHEMETER TANZANIA LIMITED

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga Aprili # 2018, alifanya ziara katika kiwanda cha kuzali...



Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga Aprili # 2018, alifanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha mita za LUKU cha Inhemeter Tanzania Limited kilichopo jijini Dar es Salaam.

Lengo la zira hiyo lilikuwa ni kuangalia utendaji kazi wa kiwanda hicho pamoja na kutatua changamoto zilizopo katika kiwanda hicho.

Akizungumza katika ziara hiyo Mshauri Mkuu wa Kiwanda hicho, Mhadisi Dkt. Adelhelm Meru alisema  kiwanda hicho kilichoanzishwa Februari mwaka huu kina uwezo wa kuzalisha mita 500,000 kwa mwaka na kusisitiza kina uwezo kwa kuzalisha hadi mita milioni moja kulingana na mahitaji ya soko.

Dkt Meru aliendelea kusema kuwa, kiwanda kimeanza kuzalisha mita kidogo na kuiomba serikali  kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya usambazaji wa miundombinu ya umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutoa oda za mita nyingi ili waanze kuzalisha mita nyingi za kutosha kulingana na soko.

"Mita tunazotengeneza zina ubora wa hali ya juu zenye kuendana na mazingira ya aina yoyote, tunaunga mkono juhudi za Serikali kuelekea kwenye uchumi wa viwanda kwa kusambaza vifaa kwa ajili ya wakandarasi wanaojenga miundombinu ya umeme nchini,"alisema Dkt. Meru.

Wakati huohuo Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo, Will Tang aliomba Serikali kutoa kipaumbele kwa matumizi ya vifaa vya umeme vinavyotengenezwa na viwanda vya ndani ya nchi.

Naye Mhandisi Luoga aliuhakikishia uongozi wa kiwanda hicho kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati inaunga mkono juhudi za kiwanda hicho na kusisitiza kuwa ipo tayari kutumia bidhaa zake katika miradi ya umeme vijijini.

"Mara baada ya kuthibitisha ubora wa bidhaa zenu, mnatakiwa kujiandaa kupokea oda kubwa kutoka TANESCO na REA kwa mwaka," aliongeza Kamishna Luoga.

Alisema katika kuhamasisha Sera yake ya Uchumi wa Viwanda, Serikali ya Awamu ya Tano inatoa kipaumbele cha matumizi ya bidhaa za ndani hususan katika miradi ya umeme nchini kwa kuwa viwanda vya ndani vitaongeza mapato, ajira na hata kurahisisha upatikanaji wa bidhaa hizo kwa bei nafuu nchini.

Akielezea hatua kadhaa zilizochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati kwenye uhamasishaji wa  uwekezaji wa viwanda vya ndani, Mhandisi Luoga alieleza kuwa, Serikali imepiga marufuku uingizaji wa nguzo za umeme kutoka nje ya nchi pamoja na bidhaa nyingine zinazopatikana hapa nchini.

"Tunataka ifike mahali mita za LUKU, transfoma, nyaya na vifaa vingine vyote vya umeme vitoke ndani ya nchi tu na kukuza uchumi wa viwanda," alisisitiza Mhandisi Luoga.

Hata hivyo Mhandisi Luoga alielekeza kampuni hiyo kukaa pamoja na Wizara, TANESCO na REA na kupanga namna ya kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme nchini.


Meneja Mwandamizi wa kiwanda cha kuzalisha mita za LUKU cha Inhemeter Tanzania Limited, Will Tang (kulia) akielezea majukumu ya kiwanda hicho kwa Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) katika ziara yake aliyoifanya katika kiwanda hicho kilichopo jijini Dar es Salaam  tarehe 03 Aprili, 2018.


Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (katikati) akitoa maelekezo kwa  uongozi wa kiwanda hicho. Kushoto ni Mshauri Mkuu wa Kiwanda hicho, Mhadisi Dkt. Adelhelm Meru na kulia ni Meneja Mwandamizi wa kiwanda hicho, Will Tang.

Mafundi wakiendelea na kazi ya kutengeneza mita katika kiwanda hicho.


Kutoka kushoto mbele Meneja Mwandamizi wa kiwanda cha kuzalisha mita za LUKU cha Inhemeter Tanzania Limited, Will Tang Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, Mshauri Mkuu wa Kiwanda hicho, Mhadisi Dkt. Adelhelm Meru na Msimamizi wa Utawala wa kiwanda hicho, Khilna Chohan wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho.


Baadhi ya mita  za LUKU zinazotengenezwa na kiwanda hicho


Mtambo maaalum wa kupima ubora wa mita katika kiwanda hicho.





COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA MITA ZA LUKU CHA INHEMETER TANZANIA LIMITED
KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA MITA ZA LUKU CHA INHEMETER TANZANIA LIMITED
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcAvM0Aym2MO47cmrfOYZs4436Mgc-uoKWYK8hT4L8U1MstKpeel93Ht52HuBJkbRGslZf85-0s89IPxQ8tqyQBjqdAyTjRaDYgNrw46VxIG4DaavEjazVG94yFvFhScz2FEZ8QdbZZNI/s640/Picha+Na+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcAvM0Aym2MO47cmrfOYZs4436Mgc-uoKWYK8hT4L8U1MstKpeel93Ht52HuBJkbRGslZf85-0s89IPxQ8tqyQBjqdAyTjRaDYgNrw46VxIG4DaavEjazVG94yFvFhScz2FEZ8QdbZZNI/s72-c/Picha+Na+1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/kamishna-wa-nishati-afanya-ziara-katika.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/kamishna-wa-nishati-afanya-ziara-katika.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy