Safari ya kuekea kilele cha Uhuru inaanza majira ya saa 5:00 usiku kwa kuianza safafri kutoka Kibo Hut. Safari ilikuwa ni usik...
Safari ya kuekea kilele cha Uhuru inaanza majira ya saa 5:00 usiku kwa kuianza safafri kutoka Kibo Hut.
Safari ilikuwa ni usiku kucha
Jua likachomoka wakati safari ikiendelea.
Kadri kulivyokucha ndivyo washiriki walivyoendelea kupata nguvu ya kuendelea na safari ya kufika Uhuru Peak.
Matumaini yakaana kuonekana baada ya alama ya Gilmans Point kuanza kuonekana.
Mdogo mdogo ndo ilikua kauli ya kuongeza morali kwa wapandaji.
Gilmans Point hatiaye washiriki wakafika lakini hii ni hatua ya kwanza bado hatua mbili ili kufika Uhuru Peak.
Miongoni
mwa waliofika Gilmans Point ni Naibuu Kamanda wa kikosi cha nchi kavu
cha jeshi la Ulinzi ,Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba.
Safari ya kueelkea Uhuru Peak ikaendelea.
Hatimaye
wapandaji wakapita kituo chha Pili ambachi ni Stella na mongoni mwa
waliofika hapa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
Balozi Charles Sanga.
a Safari ilivyoendelea kuelekea Uhuru Peak ,safu ya vilima vikiwa vyenye barafu ndio vilitawala eneo hilo.
Hatimaye
safari ya siku sita ya Wanahabari na askari wa jeshi la Ulinzi ya
kupanda Mlim Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa
Tanganyika ikafika tamati.
(Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini)
COMMENTS