Mtu aliyetuhumiwa kujaribu kuiba pikipiki aina ya Bajaj maeneo ya Coco Beach Dar es Salaam akiwa tahabani baada ya kupata kipigo cha mbw...
 |
| Mtu aliyetuhumiwa kujaribu kuiba pikipiki aina ya
Bajaj maeneo ya Coco Beach Dar es Salaam akiwa tahabani baada ya kupata
kipigo cha mbwa mwizi maeneo ya Msasani jirani na Hospitali ya CCBRT
hivi karibuni. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo kijana huyo
alikubwa na mkasa huo alipokuwa katika harakati za kukimbia na inadaiwa
alikuwa na hirizi inayomsaidia kuendelea kupumua. Askari wa Kituo cha
polisi cha Oysterbay walifanikiwa kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala na
tutawajuza kama anaendelea na hali gani. Kwa mujibu wa askari wa Kituo
hicho wamethibitisha kumfikisha hospitalini na kwa kuwa hakuna
anayemtuhumu baada ya kupata kipigo kikali watafanya mchakato wa
kumlinda mpaka atoke hospitalini. |
 |
|
 |
|
 |
|
 |
| Wakazi wa Dar es Salaam wakimwangalia kijana aliyetuhumiwa kujaribu kuiba pikipiki aina ya Bajaj baada kupata kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira. Japokuwa kuchukua sheria mkononi ni uvunjaji wa sheria pia matukio ya mauaji ya jinsi hii yameendelea kutokea bila huruma kwa jamii ya Watanzania tofauti na miaka ya nyuma ambapo watu walikuwa na utamaduni wa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ama kwa watendaji na haki kupatakana kwa watuhumiwa na wanaowatuhumu kuchukuliwa hatua ikibainika wamewasingizia. |
COMMENTS