WAZIRI MKUU: SUALA LA MISHAHARA LINAFANYIWA KAZI
HomeJamii

WAZIRI MKUU: SUALA LA MISHAHARA LINAFANYIWA KAZI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU    Simu: +255-26-216-0161/216-0167                                 Mlimwa ...

MZAZI WA DENI LA 300,000 ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI PASIPO MASHARTI YOYOTE
WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUGUMZA NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII NA WAKUU WA MAPORI YA HIFADHI ZA MISITU
WADAU WA ELIMU WAKUTANA KWA SIKU MBILI DAR ES SALAAM KUJADILI ELIMU YA JUU NCHINI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU


  Simu: +255-26-216-0161/216-0167                                 Mlimwa Kusini,
11 Barabara ya Edward Sokoine,
Nukushi:                           S. L. P. 980,
Barua-pepe: pm@pmo.go.tz                                                41193 – Dodoma,                       
Tovuti:  www.pmo.go.tz                  Tanzania.


07 Juni, 2018  
                                                                                                        
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU: SUALA LA MISHAHARA LINAFANYIWA KAZI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema suala la nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma liko Serikalini na linaendelea kushughulikiwa.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni 7, 2018) Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Bi. Susan Lyimo kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Mbunge huyo alitaka kufahamu ni kwa nini Serikali ya awamu ya tano, tangu iingie madarakani, imeshindwa kuwalipa watumishi wa umma nyongeza ya mishahara ambayo ni stahili yao ya msingi.

“Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nikuhakikishie suala la nyongeza ya mishahara liko Serikalini na Mheshimiwa Rais ameshawahikikishia wafanyakazi kuwa atawaongeza mishahara lakini siyo lazima litangazwe hadharani, na pia mshahara ni wa mtu binafsi kwa hiyo hata ikiongezwa leo huwezi kujua kwa kuwa hatujatangaza.”

“Hatuwezi kutangaza kwamba tumeongeza mishahara kwa kiwango hiki; tukishafanya hilo tayari tunaleta kupanda kwa gharama za maisha na sisi Serikali tuna mkakati wa kupunguza gharama za watumiaji kwenye masoko ili Watanzania wote wamudu kununua,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema mtumishi anapolipwa, anakuta mshahara wake kwenye akaunti yake. “Na hata tunapolipa madeni hatutangazi, lakini kila mtumishi ambaye anadai, anaona malipo yanalipwa kupitia mshahara wake na hiyo sasa inasaidia pia kuchangia hata kwenye pensheni,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali inachelea kutangaza nyongeza za mishahara hadharani ili kupunguza athari ambazo zinawapata watumishi hao na jamii kwa ujumla. “Si kwamba Serikali haikusudii kutoa nyongeza ya mishahara kwa mwaka, lakini unapotumia Mei Mosi kutangaza nyongeza ya mishahara unaleta athari kwenye jamii kwa sababu vitu vinaweza vikapanda bei, gharama hizi zikawasumbua pia na wananchi ambao hawalipwi mshahara,” amesema.

Amesema nyongeza za mwaka zinaendelea kutolewa kulingana na namna ambavyo Ofisi ya Rais (Utumishi) wameratibu. “Serikali yetu inao utaratibu wa kuwapa stahiki watumishi kadri wanavyotakiwa kuzipata na utaratibu huu unaratibiwa vizuri sana na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambako tunayo orodha ya watumishi wote nchini. Orodha hii tulianza kufanya sensa ili kutambua watumishi halali na sasa kazi hiyo imekamilika; tunaendelea na uboreshaji wa maeneo yote hayo ikiwemo na nyongeza za mwaka, nyongeza za mishahara, upandishaji wa madaraja ikiwa ni stahiki za watumishi wetu.”

Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma waendelee kuiamini Serikali wakati ikiendelea kushughulikia maslahi yao hasa kwa vile ililenga kuokoa fedha za umma zilizokuwa zikipotea kwa kuwalipa watu ambao hawastahili.

“Naomba tu niwaeleze watumishi wa umma kwamba, kwanza wawe na imani na Serikali, mpango tuliouweka unasababisha Serikali kutopoteza fedha nyingi kwa kulipa watu ambao hawastahili; lakini, baada ya kuwa tumekamilisha taratibu hizi, sasa tunaweza kuendelea kulipa stahiki za watumishi. Tumeshaanza kulipa madeni ya watumishi ambapo Mheshimiwa Rais alitenga zaidi ya shilingi bilioni 200, wiki mbili au tatu zilizopita wameendelea kulipwa kwa awamu,”.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
ALHAMISI, JUNI 7, 2018.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU: SUALA LA MISHAHARA LINAFANYIWA KAZI
WAZIRI MKUU: SUALA LA MISHAHARA LINAFANYIWA KAZI
https://lh5.googleusercontent.com/lotZeOE8wJafDWnEn7KyLfRnY_cbMKnR9vDyS4RNnRmJpIiGW9bVItk7Fg9nJymIix6DoBDpwZgWBTo6ziBXEJf8aG0AcynRMP0QSfBHLIk2HBxSg799wkK4kxTqN3MkXw9owVh0mjSmw371Lg
https://lh5.googleusercontent.com/lotZeOE8wJafDWnEn7KyLfRnY_cbMKnR9vDyS4RNnRmJpIiGW9bVItk7Fg9nJymIix6DoBDpwZgWBTo6ziBXEJf8aG0AcynRMP0QSfBHLIk2HBxSg799wkK4kxTqN3MkXw9owVh0mjSmw371Lg=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/waziri-mkuu-suala-la-mishahara.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/waziri-mkuu-suala-la-mishahara.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy