WAZIRI MKUU AMPONGEZA STEVEN MASELE
HomeJamii

WAZIRI MKUU AMPONGEZA STEVEN MASELE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU    Simu: +255-26-216-0161/216-0167                                 Mlimwa...

KAMPUNI YA PENNYROYAL TAASISI YA INTERNATIONAL VOLUNTEES OMAN YAKABIDHI VITI NA MEZA KWA SHULE ZANZIBAR
WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO
NDEGE BEACH DEVELOPMENT ASSOCIATION NA ROTARY CLUB DAR ES SALAAM YA MIKOCHENI WAUNGANA KWENYE KAMPENI YA 'MISSION GREEN'


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU


  Simu: +255-26-216-0161/216-0167                                 Mlimwa Kusini,
11 Barabara ya Edward Sokoine,
Nukushi:                           S. L. P. 980,
Barua-pepe: pm@pmo.go.tz                                                41193 – Dodoma,                       
Tovuti:  www.pmo.go.tz                  Tanzania.


05 Juni, 2018  
                                                                                                        
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU AMPONGEZA STEVEN MASELE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele na kumuahidi kwamba Serikali itampa ushirikiano ili aweze kutimiza majukumu yake.

Ametoa ahadi hiyo leo (Jumanne, Juni 5, 2018) wakati akizungumza na Mheshimiwa Masele ofisini kwake Bungeni, Dodoma. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuchaguliwa kushika wadhifa huo.

Amesema ushindi wake katika nafasi hiyo umelipa heshima kubwa Bunge na Serikali na kwamba wana matarajio makubwa kwa sababu uwepo wake, utaliongezea Taifa ushirikiano na nchi nyingine za Afrika.

"Matarajio kwa Bunge ni makubwa kwani kuna mambo ambayo tunataka ushirikiano na nchi nyingine za Afrika, hivyo uwepo wako ni muhimu katika kufanikisha utekelezaji wake."

Vilevile, Waziri Mkuu amewapongeza wabunge wengine wawiliWaheshimiwa David Silinde na Asha Abdullah Juma kwa ushirikiano wao uliochangia ushindi wa Mheshimiwa Masele.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Masele ameishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyompa na hatimaye kuibuka na ushindi huo. Amesema ushindani ulikuwa mkali kutokana na uwepo wa mataifa mengi yaliyokuwa yakiwania nafasi hiyo.

Aliahidi kutetea maslahi ya Taifa kwa muda wote atakaotumikia nafasi hiyo. “Nakuhakikishia Waziri Mkuu kwamba nitayalinda na kuyatetea maslahi ya Tanzania kwa muda wote ambao nitakuwa katika wadhifa huu.”



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.

JUMANNE, JUNI 5, 2018.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AMPONGEZA STEVEN MASELE
WAZIRI MKUU AMPONGEZA STEVEN MASELE
https://lh4.googleusercontent.com/bfsvQCfU2KzGgc0kVvckiZ19SGuWBIXYvrv7d9lac0ca_6n8wycu15S_3AMtv8wYFIE7ttO05cOiuio6yYZqRbVhJxLf3CyivQP57m6pU8KvkhvrmhEXNDXxOoPM20yZMXA5qzzEfWSUyTpASQ
https://lh4.googleusercontent.com/bfsvQCfU2KzGgc0kVvckiZ19SGuWBIXYvrv7d9lac0ca_6n8wycu15S_3AMtv8wYFIE7ttO05cOiuio6yYZqRbVhJxLf3CyivQP57m6pU8KvkhvrmhEXNDXxOoPM20yZMXA5qzzEfWSUyTpASQ=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/waziri-mkuu-ampongeza-steven-masele.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/waziri-mkuu-ampongeza-steven-masele.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy