WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA DAR, KINONDONI KUKAGUA MRADI WA TASAF
HomeJamii

WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA DAR, KINONDONI KUKAGUA MRADI WA TASAF

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairuki jana amefanya ziara katika Mkoa wa ...


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairuki jana amefanya ziara katika Mkoa wa Dar es Salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAF.


Mh. Kairuki alianza ziara hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa hua Mh. Ally Hapi.
Akiwa ofisini hapo Mh. Kairuki alisaini kitabu cha wageni na kusalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Ally Hapi, wakuu wa wilaya za Ilala, Temeke, Kigamboni na Katibu tawala wa mkoa wa Dar es salaam.

Mara baada ya kusaini kitabu cha wageni, Mh. Angela Kairuki alifanya mkutano na wakuu wa wilaya, wakurugenzi na waratibu wa TASAF Mkoa na manispaa za Dar es salaam ambapo alipokea taarifa mbalimbali za manispaa na Mkoa mradi wa kuondoa umasikini wa TASAF.

Katiba hotuba yake Mh. Kairuki amewataka waratibu wa TASAF wa Mkoa na manispaa kujipanga vema, kusimamia mradi kwa makini na kuondoa wale wote wasiostahili kupata fedha hizo katika orodha ya wanufaika wa TASAF.

Akitoa salam za Mkoa, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Ally Hapi amemshukuru Mh. Kairuki kwa ziara hiyo na kumfahamisha kuwa Mkoa wa Dar es salaam unakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mradi wa TASAF ikiwemo watu wasiostahili majina yao kuingizwa miongoni mwa wanufaika, kuingizwa kwa majina hewa, kubaguliwa kwa baadhi ya wananchi masikini kwa itikadi za kisiasa na ufuatiliaji duni unaofanywa na waratibu wa TASAF ngazi mbalimbali.

Ziara ya Mh. Angela Kairuki iligusa pia maeneo ya Kata za Kigogo na Msasani ambako Mh. Waziri alipata nafasi ya kuongea na wananchi wanufaika wa TASAF katika mikutano ya hadhara mitaa ya Kigogo Kati na Mikoroshini (Msasani).

Wananchi waliojitokeza wameishukuru serikali kwa mradi huo ambao umekua msaada mkubwa kwao katika kujikwamua na umasikini.
 
 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairukia akizungumza na mmoja wa wakazi wa Kinondoni,
mara baada ya kufanya ziara katika Mkoa wa Dar es Salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAF. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi.
 
 
 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairukia akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,akiendelea na ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAFkushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA DAR, KINONDONI KUKAGUA MRADI WA TASAF
WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA DAR, KINONDONI KUKAGUA MRADI WA TASAF
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhPAEPTqBZlCrhTLDqHhx2jnZJ6JOirWA8HkbGpojEPfaJLKm_igUVlZeqJTQfekJ_CoIxWPdMNrAu4XE8YRl1Ox-8mulBSJgYy4eqVmUOK1jxOnvsveu4DdH5SlzTvR6JRlLzRiIrqPV0/s640/1rrrr.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhPAEPTqBZlCrhTLDqHhx2jnZJ6JOirWA8HkbGpojEPfaJLKm_igUVlZeqJTQfekJ_CoIxWPdMNrAu4XE8YRl1Ox-8mulBSJgYy4eqVmUOK1jxOnvsveu4DdH5SlzTvR6JRlLzRiIrqPV0/s72-c/1rrrr.jpeg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/10/waziri-kairuki-afanya-ziara-dar.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/waziri-kairuki-afanya-ziara-dar.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy