WAZIRI JAFO: MABARAZA YA BIASHARA NI CHACHU YA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA

Na MWANDISHI WETU Uwepo wa Mabaraza ya Biashara nchini unachochea azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya ...

Na MWANDISHI WETU
Uwepo wa Mabaraza ya Biashara nchini unachochea azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati.
Haya yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati wa akifungua warsha ya viongozi wa ngazi ya Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara iliyoandaliwa na Mradi wa uboreshaji mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini  (LIC) kwa kushirikiana na TAMISEMI.
"Mabaraza ya biashara ni muhimu sana  katika kukuza uchumi wa nchi yetu hivyo ni vyema kuendelea kuimarisha vyombo hivi vya majadiliano na kupanga mipango ya pamoja kati ya Serikali na Sekta Binafsi,"alisisitiza Jafo
Warsha hiyo ya siku  mbili imelenga kuwajengea uwezo viongozi hao ili kutambua fursa na umuhimu wa mabaraza hayo katika kujenga uchumi imara.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi kwa kuandaa warsha kama hizo ambazo zinasaidia kuwaongezea na kuwajengea uwezo pamoja na kuvutia wawekezaji nchini.
"Mkoa wa Dodoma tumeweza kutumia fursa kupitia warsha hizi na zimesaidia uwekezaji kuongezeka katika sekta ya kilimo cha Alizeti na Zabibu, ambapo viwanda vidogo vidogo vya kuchakata mafuta ya alizeti na vinywaji vya mvinyo vimeweza kufunguliwa," alisisitiza Dkt. Mahenge
Naye Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TNBC), Bi. Oliver Ligula amesema kuwa semina hiyo itasaidia kuwajengea uwezo viongozi hao wa Mikoa na Wilaya pamoja na wadau mbalimbali juu ya fursa zitokanazo na mabaraza hayo ya biashara.
“Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana na TAMISEMI na wadau mbalimbali wameweza kushiriki katika semina hii ambayo itawajengea uelewa wadau na sekta binafsi ili kuweza kuleta maendeleo ya pamoja na yenye ufanisi.” alisema Bi. Ligula.
Mabaraza ya Biashara Tanzania yalianzishwa kwa mujibu wa Wakala wa Rais Na.1 wa mwaka 2001 na kuchapishwa katika Gazeti la Serikali Na.691 la tarehe 28Septemba, 2001.Madhumuni ya kuanzishwa kwa Mabaraza haya ni kuunda jukwaa la majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta ya Biashara katika kila jukwaa la utawala ili kujadiliana namna bora ya kuboresha mazingira ya boashara na uwekezaji Nchini.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR -TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya viongozi wa ngazi za Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma Juni12, 2018 Jijini Dodoma. 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya viongozi wa ngazi za Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma Juni12, 2018 Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR -TAMISEMI), Selemani Jafo akipitia nyaraka wakati wa ufunguzi wa warsha ya viongozi wa ngazi za Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma Juni12, 2018 Jijini Dodoma.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa toka TAMISEMI,Charles mhina.


Baadhi ya washiriki wa warsha ya viongozi wa ngazi za mikoa na wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma wakifuatilia hafla ya uziduzi wa warsha hiyo leo Juni12, 2018 Jijini Dodoma.

Mwezeshaji wa warsha ya viongozi wa ngazi za mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya Mikoa ya Dodoma na Kigoma, Profesa Lucian Msambichaka akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya Sekta ya Umma katika kuboresha mazingira ya biashara leo Juni12, 2018 Jijini Dodoma.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI JAFO: MABARAZA YA BIASHARA NI CHACHU YA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA
WAZIRI JAFO: MABARAZA YA BIASHARA NI CHACHU YA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3NrWAiFOjebPBmxjAZSlnzyvIUmrnXw2T9GtV6Wn0ppWp1w-mNCmeOaAoqX6-4hGtxa6VmYcm-Vl4F2rFRC80sc62sDsYKETmQ6PywvjHTG1tCKVx7i0wcpz9JqL3a67Rk1-FC0GnIzXm/s640/T1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3NrWAiFOjebPBmxjAZSlnzyvIUmrnXw2T9GtV6Wn0ppWp1w-mNCmeOaAoqX6-4hGtxa6VmYcm-Vl4F2rFRC80sc62sDsYKETmQ6PywvjHTG1tCKVx7i0wcpz9JqL3a67Rk1-FC0GnIzXm/s72-c/T1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/waziri-jafo-mabaraza-ya-biashara-ni.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/waziri-jafo-mabaraza-ya-biashara-ni.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy