TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAUNGANA NA UMMA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUHAMASISHA UELEWA KUHUSU MASUALA YA UALBINO

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli S.L.P 2643, DAR ES SALAAM Simu: +255 22 2135747/8; 2137125...




TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Barua Pepe: chragg@chragg.go.tz
Tovuti: www.chragg.go.tz

Juni 13,2018


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


SIKU YA KIMATAIFA YA KUHAMASISHA UELEWA KUHUSU MASUALA YA UALBINO

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inaungana na wadau wote wanaolinda na kutetea haki za watu wenye ualbino nchini kwenye kuadhimisha siku ya Kimataifa ya kutoa Elimu kuhusu dhana na haki za watu wenye ualbino duniani “International Albinism Awareness Day’’ tarehe 13/06/2018 ikiwa na kauli mbiu “KUANGAZA MWANGA WETU ULIMWENGUNI”. Kitaifa maadhimisho haya yatafanyika Mkoani Simiyu.
Siku hii imepitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa Azimio Na. A/HRC/RES/23/13 la terehe 18/12/2014. Tanzania ni mwanachama hai wa Baraza hilo, hivyo kama nchi tunapaswa kuishi tamko la Umoja wa Mataifa kwa vitendo na kutekeleza yaliyokubaliwa.
Tume kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini tunaendelea kutetea haki za watu wenye ualbino na kuweka msukumo wa utekelezaji wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2010.

Watanzania wanatakiwa kuachana na imani potofu za kishirikina za kuwaua, kuwanyanyapaa, kuwabagua na kuwatesa watanzania wenzetu wenye ualbino. Matukio ya ukatili, unyanyasaji, na mauaji kwa watu wenye ualbino yamepungua kwa kiasi nchini. Katika hili Tume inapenda kipekee kutambua juhudi kubwa za Serikali na wadau wote katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa watu wenye ualbino. Wenzetu wenye ualbino wanakabiliwa na changamoto zingine za kielimu, kiafya na kijamii na unyanyapaa ambapo juhudi zaidi kutoka kwa wadau wote zinahitajika.

Aidha, Tume inaiomba Serikali kuendeleza juhudi zake za kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba (sunscreen lotions) na vifaa saidizi vya kielimu kwa watu wenye ualbino ili waweze kushiriki kikamilifu katika kutoa mchango wao katika kujenga Taifa letu.

Tume inaahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote katika kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu wakiwemo watu wenye ualbino zinalindwa, zinakuzwa na kutetewa nchini.  


Imetolewa na:
SIGNED
Mary Massay
KATIBU MTENDAJI

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAUNGANA NA UMMA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUHAMASISHA UELEWA KUHUSU MASUALA YA UALBINO
TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAUNGANA NA UMMA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUHAMASISHA UELEWA KUHUSU MASUALA YA UALBINO
https://lh5.googleusercontent.com/FNZ-1zSQ7RvnhUP19RoSBf_WC4csFNnCdHfhlxzgtULJM9QKaXV1xYdAlS011i7yVzY4LSKbN06PhDtjNdENTwDKiKWpRs3KrVsYmSlXu2WN89KMG0FbYNGkqGqzNzGGcon8aBxIU4RRhGhtsA
https://lh5.googleusercontent.com/FNZ-1zSQ7RvnhUP19RoSBf_WC4csFNnCdHfhlxzgtULJM9QKaXV1xYdAlS011i7yVzY4LSKbN06PhDtjNdENTwDKiKWpRs3KrVsYmSlXu2WN89KMG0FbYNGkqGqzNzGGcon8aBxIU4RRhGhtsA=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/tume-ya-haki-za-binadamu-yaungana-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/tume-ya-haki-za-binadamu-yaungana-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy