PS 3 YABORESHA WATENDAJI WA UMMA NCHINI
Meneja mradi wa Ps 3 Mkoa wa Lindi Aloyce Mwasuka akifafanua jambo kwa  washiriki wa mafunzo hayo ya siku mbili kwa mkoa wa Dar es Salaam katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo kwa halmashauri zote za mkoa wa Dar es sallam baada ya mkoa wa Lindi kumaliza jana katika ukumbi wa klabu ya bandari manispaa ya Mtwara hii leo
HomeJamii

PS 3 YABORESHA WATENDAJI WA UMMA NCHINI

Na Abdulaziz Ahmeid Mtwara WAKATI Serikali inatarajia kuajiri katika sekta ya afya watumishi wapya 7680 (6180 wa Ofisi ya Tamisemi na ...

SBL YAZINDUA MSIMU WA PILI WA ‘’SMIRNOFF ICE BLACK DJ SEARCH’’ NDANI YA MIKOA MITANO.
RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI DAR ES SALAAM AKITOKEA ZANZIBAR OKTOBA 15,2017
RAIS ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI MJINI ZANZIBAR LEO

Na Abdulaziz Ahmeid
Mtwara
WAKATI Serikali inatarajia kuajiri katika sekta ya afya watumishi wapya 7680 (6180 wa Ofisi ya Tamisemi na 1500 wa Wizara ya afya), halmashauri nchini zimetakiwa kutumia ripoti za mfumo wa WISN plus POA iliyorahisishwa kusambaza watumishi wapya kwa kuzingatia uzito wa kazi na mahitaji kama yalivyoainishwa kwenye taarifa hizo.
Kauli hiyo imetolewa katika kikao kazi kilicholenga kuwasilisha matokeo ya uchambuzi wa mahitaji ya watumishi kwa kutumia mfumo wa WISN plus POA iliyorahisishwa kinachofanyika mkoani hapa.
Mfumo wa WISN plus POA hutumika kukokotoa mahitaji ya watumishi kwa kila kada katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia uzito wa kazi katika kituo husika.
Kwa sasa mfumo huu unatumika kwa ajili ya vituo vya afya na Zahanati tu, ukijumuisha kada mbalimbali zilizopo katika ngazi hizo za utoaji huduma ambazo ni waganga (MO), waganga wasaidizi (AMO), tabibu (CO), tabibu wasaidizi (CA), maafisa wauguzi (NO), maafisa wauguzi wasaidizi (ANO), na wauguzi (EN).
Kikao kazi hicho pia kilitumika kuzijengea uwezo Halmashauri na Mikoa ili ziweze kutumia WISN plus POA iliyorahisishwa kusambaza watumishi wapya, na katika kuomba watumishi wapya.
Akizungumza katika kikao kazi hicho  kilicholenga kuwasilisha matokeo ya zoezi la kubaini mahitaji ya watumishi kwa kutumia mfumo wa WISN PLUS POA iliyorahishwa Mganga Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam  alisema  mfumo huo ni toleo jipya unaowezesha kutumia taarifa kutoka mfumo wa DHIS 2 kwa ajili ya kukokotoa mahitaji ya watumishi, hivyo kupunguza gharama za kutembelea vituo kwa ajili ya kukusanya taarifa.
Kikao kazi hicho kilishirikisha  Maafisa Utumishi wa Mikoa na Halmashauri, Waganga wakuu wa wilaya, Makatibu wa Afya wa Mikoa na Wilaya, Waratibu wa MTUHA wa Halmashauri na Wadau wa Maendeleo wa Mradi wa PS3.
Mfumo huo ni sehemu ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo katika Sekta ya Umma – “Public Sector System Strengthening – (PS3) unaotekelezwa kwa ufadhili awatu wa Marekani kupitia USAID.


Tayari Halmashauri za mkoa wa lindi,Ruvuma na mtwara zimeshapatiwa mafunzo kwa kanda ya mtwara ikifuatiwa na mikoa ya Tanga na Pwani.


Mwezeshaji wa mafunzo ya Wisn plus Poa, Christina Godfrey, ambae ni afisa program, sera  na uraghibishi PS 3  akitoa elimu juu matumizi ya Tehama ikiwa ni  kuwajengea uwezo maafisa utumishi na wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa wa Ruvuma  juu ya namna bora ya upangaji wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia mahitaji.




Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: PS 3 YABORESHA WATENDAJI WA UMMA NCHINI
PS 3 YABORESHA WATENDAJI WA UMMA NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0AorGYKxg87uycVDDW-yeYJ7VghUV0q5-imtwAxjWBFX1WaUIGGkW_gMKvXkM04-lGVTn5zel2ANy6T_Aq6gNp4Oe_M8f82Hoo0la2Dz1rqRALJkLC01tbLINsaF0Ue3mCGKR9XWARBw/s640/_20171220_025955.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0AorGYKxg87uycVDDW-yeYJ7VghUV0q5-imtwAxjWBFX1WaUIGGkW_gMKvXkM04-lGVTn5zel2ANy6T_Aq6gNp4Oe_M8f82Hoo0la2Dz1rqRALJkLC01tbLINsaF0Ue3mCGKR9XWARBw/s72-c/_20171220_025955.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/ps-3-yaboresha-watendaji-wa-umma-nchini.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/ps-3-yaboresha-watendaji-wa-umma-nchini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy