PROFESA MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KAMBI YA SOGA YA UJENZI WA RELI YA KATI

WAZIRI wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ...



WAZIRI wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa Kituo cha Soga, Wilayani Kibaha, mkoani Pwani ili kujiridhisha na utekelezaji wa masharti ya mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki kwa ajili ya kufanya kazi saa 24 ili kukamilisha ujenzi wa reli hiyo kwa wakati.

Katika ziara hiyo Profesa Mbarawa, licha ya kuwakuta baadhi ya Makandarasi na wasimamizi wakiwa kazini pia akabaini kuwepo kwa wasimamizi wachache wasiotosheleza na hivyo kuagiza kuongezwa kwa wasimamizi kutoka watatu waliokuwepo hadi kufikia 15.

"Natoa agizo kwa uongozi wa Shirika la Reli nchini (TRC), kuongeza wasimamizi wa mradi huo haraka iwezekanavyo ili kazi ya usimamizi iweze kufanyika kwa umakini na kwa muda wa saa 24", amesisitiza Prof.Mbarawa .

Aidha Waziri Prof. Mbarawa, amesema ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge)’SGR’ kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa KM 300 ambapo kati ya hizo KM 205 ni eneo la njia ya reli na nyingine 95 ni za kupishana na mradi huo utagharimu kiasi cha Shilingi Trilioni 2.79.

Profesa Mbarawa ameongeza reli hiyo ya kisasa inayotumia umeme itakuwa na uwezo wa kusafiri kwa mwendokasi wa KM 160 kwa saa kwa treni ya abiria na , treni ya mizigo itakuwa na uwezo wa kusafiri kwa KM 120 kwa saa na kubeba mizigo tani 10,000 kwa wakati mmoja.

Pamoja na hayo amesema kuwa kipande cha reli kingine kitakachojengwa ni kutoka Morogoro-Makutupola chenye urefu wa KM 422, na hivyo kufanya jumla ya KM 722 kutoka mkoani Dar es Salaam hadi Makutupora na mradi huo utagharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi Trilioni 7 na fedha zote zitagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100.

Hata hivyo ametumia fursa hiyo kumtaka mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo kupitia Meneja mradi, Kemal Artuz kuogeza kasi ya ujenzi ili kufikiwa makubaliano ya kukamilishwa kwa wakati ili kuwezesha watanzania kunufaika na matunda hayo.

Kwa upande wake Mhandisi Msimamizi wa Mradi huo, Josephat Rutaihwa amesema, kazi za ujenzi huo zinaenda kwa kasi kutokana na vifaa kuwepo eneo la mradi.

Mhandisi huyo amemhakikishia Waziri kuwa kazi hiyo inakwenda kama ilivypoangwa na kwamba mradi huo utakamilishwa ndani ya mkataba Novemba 2, 2019.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa (kulia) akipatiwa maelezo na Meneja mradi wa Kampuni ya Yapi Merkezi ya nchini Uturuki, Kemal Artuz kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa Standard Gauge (SGR) jana usiku eneo la kambi ya Soga, iliyopo wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu  hatua mbalimbali zilizofikiwa za maendeleo ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa Standard Gauge (SGR) jana usiku eneo la kambi ya Soga, iliyopo wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.



Muonekano wa sehemu ya tuta la reli ya kisasa lililojengwa eneo la soga Wilayani kibaha mkoani Pwani. Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Novemba, 2019.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: PROFESA MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KAMBI YA SOGA YA UJENZI WA RELI YA KATI
PROFESA MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KAMBI YA SOGA YA UJENZI WA RELI YA KATI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLYFm_qUl7K-zxJZCNcadrdBRm7zyeEr_idWzXJONYMtwfFqZYmmBHDUVsCRfQEce3zP6EMkBp88_7MjQXBzcJJlX0jrcULpCdKtZfFxBGnqS5Fn325L0t3cIQm9xxBWRwHpe6cf1qs00/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLYFm_qUl7K-zxJZCNcadrdBRm7zyeEr_idWzXJONYMtwfFqZYmmBHDUVsCRfQEce3zP6EMkBp88_7MjQXBzcJJlX0jrcULpCdKtZfFxBGnqS5Fn325L0t3cIQm9xxBWRwHpe6cf1qs00/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/profesa-mbarawa-afanya-ziara-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/profesa-mbarawa-afanya-ziara-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy