06/06/2018 KIDATU, MOROGORO Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewataka Wakuu wa Polisi Wilaya ma OCD na Maofisa Opereshe...
06/06/2018 KIDATU, MOROGORO
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewataka Wakuu wa Polisi Wilaya ma OCD na Maofisa Operesheni kuhakikisha wanafanyakazi zao kwa misingi ya kukutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia pia kwa kuzingatia weledi na mafunzo waliyoyapata.
IGP Sirro amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya utayari ya kuwajengea uwezo wakuu hao yaliyofanyika kwa muda wa wiki nne katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu, kilichopo mkoani Morogoro ikiwa ni muendelezo wa mkakati kuwajengea uwezo na mbinu mbalimbali za medani.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu Naibu Kamishna wa Polisi DCP Mpinga Gyumi, amesema kuwa hadi sasa jumla ya wanafunzi 1223 wamepatiwa mafunzo ya utayari yatakayowasaidia katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu.
Naye Naibu Kamishna wa Polisi mstaafu DCP Venance Tossi, ambaye pia ni mshauri mwelekezi wa Jeshi hilo amesema kuwa, kwa sasa Jeshi la Polisi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mafunzo mbalimbali yanayoendelea kufanyika katika Jeshi hilo.

COMMENTS