MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA URAFIKI NA KUKUTA MADUDU

SERIKALI imesema hairidhiki na ubia unaoendeshwa kwenye Kiwanda cha Nguo cha Urafiki. Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Maja...



SERIKALI imesema hairidhiki na ubia unaoendeshwa kwenye Kiwanda cha Nguo cha Urafiki.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Juni mosi, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wafanyakazi wa kiwanda hicho mara baada ya kukagua mitambo mbalimbali kwenye kiwanda hicho.

“Serikali haturidhiki na ubia huu, na huyu mbia aelewe kwamba Serikali haturidhishwi na ubia huu wala kinachoendelea hapa kiwandani,” amesema huku akishangiliwa kwa nguvu na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aongoze kikao baina ya wabia hao na menejimenti ya kiwanda na apewe taarifa hiyo leo saa 12 jioni baada ya kufuturu.

“Ubia wenu hauna tija. Kwa hiyo wewe Msajili wa Hazina na huyo mwekezaji, nikitoka hapa, mbaki mfanye kikao na mnipe majibu leo saa 12 jioni. Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Mkuu wa Mkoa muongoze mjadala huo na nikitoka kufuturu mniambie maazimio yenu, na kama haiwezekani, mvunje kabisa ubia huo ili tujue hatuna mbia tutafute mbia,” amesema.

Waziri Mkuu amesema wabia wakuu wa kiwanda hicho ni Msajili wa Hazina na kampuni ya Changzhou State owned Textile Assets Operations kutoka China na kwamba Serikali ilipoamua kukaribisha uwekezaji ilitarajia kupata mtaji, teknolojia na ajira za kutosha lakini hali ya sasa ni kinyume kabisa.

“Hatuwezi kuvumilia, tunasema tuna mbia mwenye mtaji, hakuna mtaji; tulisema tunataka mbia mwenye kuleta teknolojia mpya, hakuna teknolojia; tulisema aendeshe shughuli hii kukiwa na ajira endelevu, hizo ajira hakuna; halafu tubaki tunamwangalia tu. Bora atuambie amekwama, aondoke, tutangaze vinginevyo,” amesema.

“Tulikopa mtaji lakini Tanzania hizo hela hazijaja, tunataka majibu ya fedha hizo; kama fedha iliyokopwa kwenye Benki ya Exim ya China ingeletwa nchini tungeweza kuziba mapengo na kusaidia kiwanda kiweze kufanya kazi. Sasa kwa sababu fedha hiyo haijaja nchini, tunataka maelezo fedha hiyo iko wapi?” amesisitiza.

“Mitambo iliyonunuliwa na mwekezaji miaka mitano au sita iliyopita haifanyi kazi tangu ilipoletwa nchini, nataka majibu, je mitambo hii ilinunuliwa ikiwa mizima au vipi; na tena mmeng’oa mashine kwenye ma-godown matatu, nimeambiwa mlikuwa na nia ya kuleta mashine mpya, lakini sasa ni miaka mitano, je mashine zile zote zimeenda wapi, na kama mmeuza ameuziwa nani? Mkae mjadili na leo hii mniletee majibu yote haya,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kiwanda hicho ni matokeo ya urafiki wa China na Tanzania na kina historia ndefu na mahusiano ya muda mrefu. “Asiingie mtu akatuharibia, na tunataka mahusiano yetu na China yaendelee. Amesema baada ya kupokea taarifa hiyo, Serikali itakaa na Balozi wa China ili itafutwe suluhisho.

Waziri Mkuu amewataka watumishi wa kiwanda hicho walioko likizo na wale waliopo kazini wawe wavumilivu wakati Serikali ikiendelea kutafuta dawa ya matatizo yao.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemtaka Meneja Rasilmali Watu na Utawala wa kiwanda hicho, Bw. Edwin Nkwanga aandae orodha ya watumishi wote yenye kuonyesha kila mtumishi analipwa nini na aifikishe kwake haraka.

“Hapa kuna watu wanalipwa sh. milioni saba hadi 10 na wengine wanalipwa sh. 120,000. Niletee orodha yenye kuonyesha jina, cheo na kiwango cha mshahara, lakini pia uonyeshe anapata stahili zipi, kama ni posho ya nyumba, maji au umeme,” amesema.

Amesema nia ya Serikali ni kutaka kupanga upya mishahara yao ili waweze kupatikana watumishi wa kutosha.

Wakati akikagua kiwanda hicho, Waziri Mkuu alielezwa kwamba kuna mashine 88 ambazo ziling’olewa kwenye kiwanda hicho na hazijulikani zimepelekwa wapi.

Mapema, akitoa taarifa fupi ya kiwanda hicho, Naibu Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Shadrack Nkelebe alisema kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba 2017 ili kufanya ukarabati na kimeshindwa kuendelea nao kwa sababu ya madeni.


“Kiwanda kilikuwa na watumishi 3,000 lakini sasa hivi wamebakia 726 baada ya wengine kupunguzwa na kulazimishwa kwenda likizo licha ya teknolojia kubakia ni ileile. Kiwanda kinakabiliwa na changamoto nyingi lakini kwa sehemu kubwa ni za kutengeneza. Tumepigana vita katika kujenga uchumi wa Taifa kupitia kiwanda hiki, lakini tumekwama. Tunahitaji nguvu ya ziada ili tutoke hapa,” alisema.
PMO_3842
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam baada ya kukagua kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarest Ndikilo. 
PMO_3847
 Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipozungumza nao kiwandani hapo, Juni1, 2018.PMO_3720
 Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mhandisi Mkuu wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam, Khamis Mazugo (kushoto)  kuhusu mitambo ya kiwanda hicho iliyokoma kufanya kazi wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana.
PMO_3750
PMO_3752
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipita katika eneo zilipong'olewa mashine za kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana.
PMO_3770
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Meneja Mkuu wa kiwanda cha nguo cha Urafiki, Shadrack Nkelebe kuhusu mashine za kutengeneza  nyuzi za pamba wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA URAFIKI NA KUKUTA MADUDU
MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA URAFIKI NA KUKUTA MADUDU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgi6WvbaQ0CeQLXCP44scs1MVq9P_TliwB-Nj6JPimlhNY98TEvORAzwUE1bUQn9_lnQM5WS-W5QEKjFAcplqtU9YgpppSJnwchlwQynG4LBJ2pKr-yy8XDMoiGYqm6GwfAt9AcRHIhKvg/s640/PMO_3842.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgi6WvbaQ0CeQLXCP44scs1MVq9P_TliwB-Nj6JPimlhNY98TEvORAzwUE1bUQn9_lnQM5WS-W5QEKjFAcplqtU9YgpppSJnwchlwQynG4LBJ2pKr-yy8XDMoiGYqm6GwfAt9AcRHIhKvg/s72-c/PMO_3842.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/majaliwa-atembelea-kiwanda-cha-urafiki.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/majaliwa-atembelea-kiwanda-cha-urafiki.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy