DOKTA KIJAJI AFANYA ZIARA MITAANI JIJINI DODOMA KUKAGUA MASHINE ZA EFD NA KUBAINI BAADHI YA WAFANYABIASHARA HAWAZITUMII
HomeJamii

DOKTA KIJAJI AFANYA ZIARA MITAANI JIJINI DODOMA KUKAGUA MASHINE ZA EFD NA KUBAINI BAADHI YA WAFANYABIASHARA HAWAZITUMII

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amefanya ziara katika mitaa ya Jiji la Dodoma, kuk...




Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amefanya ziara katika mitaa ya Jiji la Dodoma, kukagua upatikanaji wa huduma ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs), ambazo mfumo wake ulipata hitilafu hivi karibuni ambao hivi sasa umetengemaa na kubaini kuwa licha ya hitilafu iliyotokea, wafanyabiashara wengi katika jiji hilo hawazitumii ipasavyo mashine hizo.
Dkt. Kijaji aliyeambatana na Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Elijah Mwandumbya, amewaonya wafanyabiashara kote nchini wanaokiuka masharti ya matumizi ya mashine hizo kuacha vitendo hivyo mara moja na kuiagiza TRA kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara wasiotoa risiti za kieletroniki baada ya kuuza bidhaa zao.
"Wanauza mauzo yao vizuri lakini hawatoi risiti, tumeongea nao kuwaeleza kuwa wanapaswa kutoa risiti wanapouza bidhaa na huduma zao kwani suala hilo ni la kisheria, ni lazima litekelezwe" alionya Dkt. Kijaji
Alisema kuwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla wanapaswa kuelewa kuwa maendeleo ya nchi hayawezi kupatikana bila kukusanywa kwa kodi sahihi.
"Tunadai maji, huduma za afya, barabara nzuri, bila kukusanya na kulipa kodi haiwezekani tukayafikia haya malengo ya kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati" aliongeza Dkt. Kijaji
Kwa Upande wake, Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA Bw. Elijah Mwandumbya, amesema kuwa wafanyabiashara wasiotumia ipasavyo mashine za EFD watakabiliwa na adhabu kali inayofikia shilingi milioni nne na nusu kwa kutokutoa risiti huku mteja akikabiliwa na faini ya shilingi elfu thelathini kwa kutokudai risiti inayolingana na thamani ya bidhaa alizonunua.
"Ni kosa kuwa na mauzo ambayo hujayatolea risiti na ndio maana tunawapa fursa hii waweze kuweka kumbukumbu zao sawasawa kwa sababu tumegundua baadhi yao wanayo mauzo lakini hawajatoa risiti" aliongeza Bw. Mwandumbya.
Bw. Mwandumbya ameeleza kuwa ukaguzi wao umeonesha kuwa zaidi ya asilimia 90 ya mashine za kieletroniki zinafanyakazi ipasavyo baada ya kutengemaa kwa mfumo wa kuchakata taarifa za mauzo kwa njia ya kieletroniki uliopata hitilafu tangu Mei 11 mwaka huu na kusababisha baadhi ya mashine hizo za EFD kutofanyakazi.
Aliwataka wafanyabiashara kuingiza mauzo yote waliyoyafanya katika kipindi chote ambacho kulikuwa na hitilafu ya kimfumo katika mashine ya EFD na kutoa risiti moja ya mauzo hayo ili yaweze kutambulika katika mfumo wa mapato wa TRA kwa ukadiriaji sahihi wa kodi za biashara zao.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DOKTA KIJAJI AFANYA ZIARA MITAANI JIJINI DODOMA KUKAGUA MASHINE ZA EFD NA KUBAINI BAADHI YA WAFANYABIASHARA HAWAZITUMII
DOKTA KIJAJI AFANYA ZIARA MITAANI JIJINI DODOMA KUKAGUA MASHINE ZA EFD NA KUBAINI BAADHI YA WAFANYABIASHARA HAWAZITUMII
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3BcOwe-ixDzDk7AyCoGyDyU1HyEvKwCejuvJm-uCWbqc6irKBpdn1KIODFEhQkM3jXmMpnG2D9RrmcTLZOt9AENBNDCotShhqFefXY9705vu9LX_ao4GXoz293yYH7nfM1_koYdrV4P8/s400/Dk+Ashatu+Kijaju.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3BcOwe-ixDzDk7AyCoGyDyU1HyEvKwCejuvJm-uCWbqc6irKBpdn1KIODFEhQkM3jXmMpnG2D9RrmcTLZOt9AENBNDCotShhqFefXY9705vu9LX_ao4GXoz293yYH7nfM1_koYdrV4P8/s72-c/Dk+Ashatu+Kijaju.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/dokta-kijaji-afanya-ziara-mitaani.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/dokta-kijaji-afanya-ziara-mitaani.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy