Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amewasili katika Ofisi za Makao makuu ya Wizara zilizoko ndani ya Chuo Kikuu cha Dodom...
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amewasili katika Ofisi za Makao makuu ya Wizara zilizoko ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma na kulakiwa na watumishi wa Wizara walioko makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.
Prof Kabudi aliapishwa tarehe 24/03/2017 Ikulu jijini Dar es Salaam kuchukua nafasi hiyo baada ya Mhe.Rais kufanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaaziri ambapo Dkt. Harrison Mwakyembe alihamishiwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Nje ya Ofisi za Wizara, Profesa Palamagamba Kabudi alilakiwa na Naibu Katibu Mkuu, Amon Mpanju, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Aloyce Mwogofi, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma na wafanyakazi wengine wa Wizara waliopo Makao Makuu ya Serikali mjini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Jaji mfawidhi Kanda ya Dodoma Mhe. Mwanaisha Kwariko. Kushoto kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu, Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana wafanyakazi wa wizara hiyo alipowasili Wizarani hapo mjini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi akisikiliza maelezo mbalimbali alipokutana na watendaji wa Wizara na katika ukumbi wa mikutano Wizarani mjini Dodoma.
COMMENTS