DKT TIZEBA AMALIZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI SINGIDA ATUA TABORA

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye kikao kazi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.  Picha Zote Na Mathias ...



Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye kikao kazi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida. Picha Zote Na Mathias Canal, WK. Juzi 8 Juni 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Kushoto) na Mkuu wa Wilya ya Singida Mhe Elias Tarimo wakifatilia kikao cha kazi kilichoongozwa na waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba, Juzi 8 Juni 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza jambo mbele ya waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba alipotembelea ofisi ya Mkoa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili, Juzi 8 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye kikao kazi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida. Juzi 9 Juni 2018.

Na Mathias Canal-WK, Tabora

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemaliza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Singida na tayari amewasili mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku moja hapo kesho 10 Juni 2018.

Akiwa Mkoani Singida Mhe Dkt. Tizeba ametembelea vituo mbalimbali vya ukusanyaji wa pamba na kujionea msimu wa ununuzi wa pamba katika Wilaya ya Ikungi na Iramba.

Miongoni mwa mambo ya msisitizo katika maeneo yote hayo ni pamoja na kuwashauri wakulima kutouza pamba chafu kwa kudhani kuwa watapata kilo nyingi kwani jambo hilo linafifihisha soko la zao hilo kwa wanunuzi.

Katika hatua nyingine ametoa onyo kwa viongozi wa vyama vya ushirika AMKOS kutojihusisha na ubadhilifu wa fedha za wakulima huku akielekeza kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa wale wote waliobainika kuiba fedha za wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, ametangaza neema kwa wakulima wa pamba kote nchini kuwa msimu ujao wa kilimo wa mwaka 2018/2019 wakulima watapatiwa mbegu na dawa bure pasina malipo.

Akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Tizeba amewasisitiza watendaji wote mkoani humo kutoa ushirikiano mahususi kwa wakulima ili kuongeza tija katika uzalishaji wa zao la pamba na mazao mengine yakiwemo mahindi, mtama, alizeti N.k

Zao la pamba ni miongoni mwa mazao ya biashara yanayolimwa katika mkoa wa Singida, Katika msimu huu wa mwaka 2017/2018, mkoa ulipokea mbegu bora za pamba aina ya UKM 08 tani 381.48 na kusambazwa kwa wakulima ambapo jumla ya ekari 35,889 zilipandwa. Aidha, sumu chupa 137,970 zimesambazwa kwa wakulima na mabomba ya kunyunyizia sumu 365 yamesambazwa pia.

Pia amesisitiza kuwa uongozi wa mkoa huo unapaswa kujipanga kikamilifu kusimamia ununuzi wa pamba kupitia utaratibu uliowekwa wa kuvitumia Vyama vya Ushirika vya Kilimo na Masoko (AMCOS) pamoja Vyama vya Awali vya Ushirika  (Pre Cooperative Societies).

Katika mkoa huo jumla ya AMCOS 36 na “Pre Cooperatives” 20 zitahusika katika ununuzi wa zao la pamba katika msimu huu wa kilimo wa mwaka 2017/2018.

Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt Rehema Nchimbi alisema kuwa mkoa huo ulikuwa na matarajio ya awali ya mavuno kwa tani 21,533.4 ambapo matarajio haya yameshuka mpaka kufikia tani 14,015.2 zinazotarajiwa kuvunwa kutokana na athari za wadudu waharibifu.

Alisema jumla ya vituo vitakavyotumika kukusanya na kununua pamba ni 117 ambavyo vimesambaa katika maeneo yote yanayolima pamba yaliyopo katika Halmashauri saba za Mkoa huo.

Aliongeza kuwa maghala yatakayotumika kununulia pamba katika vituo hivyo  yamesafishwa na kufukiziwa sumu ya kuuwa wadudu. Kampuni iliyoruhusiwa kununua pamba katika Mkoa huo ni BioSustain (T) LTD ambayo ni mdau mkubwa wa kilimo cha zao la pamba katika mkoa wa Singida kwani imewekeza kiwanda cha kuchambua pamba kilichopo Manispaa ya Singida.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT TIZEBA AMALIZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI SINGIDA ATUA TABORA
DKT TIZEBA AMALIZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI SINGIDA ATUA TABORA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhA-vzJ3e8Yu2Sck0X26waDduswIiA0RaAiCA8KXpcWppa8SLe7ANfPZwche9wFaKNNC1oh8CVcF0JIIZQMzBuSCjuNXGs7t7gTm8pGzoA8fdHTC_qJDjikCmRhAWaR971ZAQRzbUoYY4A-/s1600/DSC_0745.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhA-vzJ3e8Yu2Sck0X26waDduswIiA0RaAiCA8KXpcWppa8SLe7ANfPZwche9wFaKNNC1oh8CVcF0JIIZQMzBuSCjuNXGs7t7gTm8pGzoA8fdHTC_qJDjikCmRhAWaR971ZAQRzbUoYY4A-/s72-c/DSC_0745.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/dkt-tizeba-amaliza-ziara-ya-kikazi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/dkt-tizeba-amaliza-ziara-ya-kikazi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy