DKT TIZEBA AAGIZA KUKAMATWA KIONGOZI WA AMKOS ALIYEFUJA MILIONI 23

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramb...



Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba  akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na kujionea ununuzi wa pamba, Picha Zote Na Mathias Canal, WK
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba  akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na kujionea ununuzi wa pamba, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuely Lwehahula.
Kituo cha ukusanyaji na ununuzi wa pamba katika kijiji na Kata ya Msai, Wilayani Iramba

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuely Lwehahula akitoa salamu za shukrani kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwa kufanya ziara ya kuwatembelea  wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na kujionea ununuzi wa pamba, 

Na Mathias Canal-WK, Singida

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Mrakibu wa polisi Wilaya ya Iramba ASP Magoma Mtani kumkamata aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha ushirika (AMKOS) Msai.

Waziri Tizeba ametoa agizo hilo jana 9 June 2018 Mara baada ya kutembelea kitongoji cha Kati, Msai na Mtoa akiwa katika ziara ya kikazi ya Siku mbili kwa ajili ya kutembelea vituo vya ununuzi wa pamba na kujionea msimu wa ununuzi wa zao hilo katika vijiji hivyo.

Dkt Tizeba amelaani vikali ufujaji huo wa fedha za wakulima huku akimtaja Paul Ramadhan Kurwa kuhusika na ufujaji huo wa shilingi milioni 23 huku akiendelea kuonekana mtaani pasina kuchukuliwa hatua za kisheria.

"Wakati muelekeo wa serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli ukijipambanua kutaka kuboresha maisha ya watanzania kupitia Kilimo lakini kuna watu wanataka kurudisha nyuma juhudi hizo, hakika tutawapa kibano kweli kweli hakuna utani kwenye fedha za wananchi" Alikaririwa Dkt Tizeba

Mhe Tizeba ametoa siku moja kukamatwa kwa mwizi huyo na kufikishwa mahakamani ili awe mfano kwa wezi wengine wasio kuwa na haya wala soni.

Aidha, amewataka wananchi katika msimu huu wa uuzaji na ununuzi wa Pamba kutouza Pamba zenye uchafu wakidhani wataongeza idadi ya kilo kwani kufanya hivyo ni kufifihisha juhudi zao wenyewe jambo ambalo halina tija.

Sambamba na hayo pia amewaondoa hofu wakulima kote nchini kuwa serikali ya awamu ya tano inatekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi yenye mkataba na wananchi katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuely Lwehahula amempongeza Waziri Tizeba kwa kutembelea maeneo mbalimbali ili kujionea ununuzi wa Pamba huku akiwasihi wananchi wilayani humo kulima kiasi kikubwa cha Pamba msimu ujao kwani mbegu na madawa ya kuulia wadudu vitatolewa bure kuanzia msimu ujao wa mwaka 2018/2019.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT TIZEBA AAGIZA KUKAMATWA KIONGOZI WA AMKOS ALIYEFUJA MILIONI 23
DKT TIZEBA AAGIZA KUKAMATWA KIONGOZI WA AMKOS ALIYEFUJA MILIONI 23
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhruG2zisbdZa1i6ywvdQxTnxaDjHVMD7EdntV_vMqUpZ1P2iyfeRa7ZpsYVDWur0EbIElsNBTKSbY6DO7yb1aCk0fip5ndzwWzPZ-05dBU6sSTUZT9QeIzLiqt3aUlNa4ketlFfxNJ-j6v/s640/DSC_0780.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhruG2zisbdZa1i6ywvdQxTnxaDjHVMD7EdntV_vMqUpZ1P2iyfeRa7ZpsYVDWur0EbIElsNBTKSbY6DO7yb1aCk0fip5ndzwWzPZ-05dBU6sSTUZT9QeIzLiqt3aUlNa4ketlFfxNJ-j6v/s72-c/DSC_0780.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/06/dkt-tizeba-aagiza-kukamatwa-kiongozi-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/dkt-tizeba-aagiza-kukamatwa-kiongozi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy