Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya CBA, Dk Gift ...
 |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya CBA, Dk Gift Shoko (wa tatu kushoto) wakiwaogoza wateja wa benki hiyo kupakua futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwenye hafla iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. |
 |
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), Dk. Gift Shoko akizungumza na baadhi ya wateja wakubwa wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati benki hiyo ilipoandaa futari mahsusi. Kati ya mengi aliyoeleza, Shoko aliwahakikishia wateja wa benki hiyo jitihada madhubuti na endelevu zinazoendelea kufanywa na benki ya CBA kwa kuboresha huduma na bidhaa zake wakati wote. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba kama mgeni rasmi. |
 |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba akiongea na wageni walioshiriki katika futari hiyo. |
 |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba (wa tatu kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya CBA, Dk Gift Shoko (wa tatu kulia) wakiwa katika picha pamoja baadhi ya wateja na viongozi wa benki hiyo. |
COMMENTS