WAZIRI WA KILIMO DKT. TIZEBA HAKUTARAJIWI KUWA NA UPUNGUFU WA SUKARI NCHINI

Na Bashiri Salum, Dodoma Serikali imeagiza sukari kiasi cha tani 70,354.35 kutoka nchi za nje lengo likiwa ni kujipanga ili kuhakikis...



Na Bashiri Salum, Dodoma

Serikali imeagiza sukari kiasi cha tani 70,354.35 kutoka nchi za nje lengo likiwa ni kujipanga ili kuhakikisha kuwa hapatokei upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni waziri  wa kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa tani 60,539.35 ya sukari itaanza kuingia hapa nchini katikati ya mwezi Mei 2018 ambapo kiasi kilichobaki cha tani 9,815 kitaingia mwezi  June mwaka 2018.

Aidha  Dkt. Tizeba amefafanua kwamba hakutarajiwi kuwa na upungufu wa sukari hapa nchini  kwa sababu hadi kufikia tarehe 10 mei 2018 katika maghala ya wazalishaji na wafanyabiashara kulikuwa na tani 78,147.67 za sukari na kiasi kingine  tani 25,441.25 kipo Bandarini .

Kwa kiasi cha sukari ambacho tayari kipo hapa nchini kikijumlishwa na kiasi ambacho kitaingia hivi karibuni kutoka nje ya nchi ni dhahiri kwamba  nchi haiwezi kupata upungufu wa bidhaa hiyo, alisema Mhe.Waziri.

Awali Dkt.Tizeba  alisema kwamba mahitaji ya sukari nchi nzima ni tani 630,000 ambapo kati ya hizo, tani 145,000 ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani na tani 485,000 ni kwajili ya matumizi ya kawaida.

Hata hivyo mapitio yanaonesha kwamba  msimu wa mwaka 2017/18  viwanda vya ndani vilizalisha tani 306,226  za sukari kwa matumizi ya kawaida  ambapo mwisho wa msimu huu uzalishaji umefikia tani 307,481.76 aliongezea Dkt. Tizeba.

Akimalizia taarifa yake Mhe. Tizeba amebainisha kuwa kwa kiasi ambacho sukari imeagizwa kutoka nje Pamoja na viwanda vya ndani inadhihirisha kwamba hakutakuwa na upungufu wa aina yeyote ya sukari hapa nchini na ikizingatiwa  kuwa viwanda vitaanza uzalishaji mwingine mwezi mei ambapo ukarabati (services ) itakuwa imekamilika .

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI WA KILIMO DKT. TIZEBA HAKUTARAJIWI KUWA NA UPUNGUFU WA SUKARI NCHINI
WAZIRI WA KILIMO DKT. TIZEBA HAKUTARAJIWI KUWA NA UPUNGUFU WA SUKARI NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnB2YMaSayCBwfZox3F3YDXoEMQP2pj4PeZmr3soVKX3Ai8lgf1TCcd_SQCkHpZn6nxfRGt4kWbn-Mv8kEx2O7V9d0VLL6A8WwBcEZd2Z69jcXx6uxarGR5HBl50JFU1fr1RWL8WdcLnQ/s400/tizeba1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnB2YMaSayCBwfZox3F3YDXoEMQP2pj4PeZmr3soVKX3Ai8lgf1TCcd_SQCkHpZn6nxfRGt4kWbn-Mv8kEx2O7V9d0VLL6A8WwBcEZd2Z69jcXx6uxarGR5HBl50JFU1fr1RWL8WdcLnQ/s72-c/tizeba1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-wa-kilimo-dkt-tizeba.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-wa-kilimo-dkt-tizeba.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy