WAZIRI KALEMANI ATEMBELEA VITUO VYA KUPOZA UMEME DAR ES SALAAM NA KIWANDA CHA MITA CHA INHEMETER TANZANIA LIMITED

Tarehe 30 Mei, 2018 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alifanya ziara katika vituo vya kupoza umeme vya Kurasini, Kigamboni  na kiwan...


Tarehe 30 Mei, 2018 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alifanya ziara katika vituo vya kupoza umeme vya Kurasini, Kigamboni  na kiwanda cha kutengeneza mita za LUKU cha Ihemeter Tanzania Limited. Lengo la ziara yake katika vituo vya kupoza umeme lilikuwa ni kuangalia maendeleo ya ukamilishwaji wa vituo husika. Akiwa katika vituo vya Kurasini na Kigamboni Waziri Kalemani alielekeza kuhakikisha ujenzi wake unakamilika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu. Aidha, alielekeza ujenzi wa majengo ya kituo kipya cha Kigamboni kilichopo Dege jijini Dar es Salaam kukamilika mwezi Julai mwaka huu na kusisitiza mradi mzima kukamilika mapema DIsemba mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kalemani akizungumza na wananchi wa Mbutu wilayani Kigamboni alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linawaunganishia wananchi huduma ya umeme mara moja ili kuondokana na changamoto ya ukosefu wa umeme.

Wakati huohuo, Waziri Kalemani akiwa katika kiwanda  cha kutengeneza mita za LUKU cha Ihemeter Tanzania Limited, alipongeza uzalishaji wa kiwanda hicho ambao umefikia hadi mita milioni moja kwa mwaka na kulitaka Shirika la TANESCO pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya usambazaji wa miundombinu  ya umeme vijijini chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutumia mita hizo baada ya kujiridhisha na ubora wake. Aliitaka kampuni ya Ihemeter Tanzania Limited kuongeza uzalishaji wa mita zenye ubora na kupunguza gharama ili waweze kusambaza mita nyingi zaidi. Aidha aliitaka kampuni ya Inhemeter kuanza kuzalisha bidhaa za aina nyingine kama nyaya ili vifaa vya umeme viweze kununuliwa nchini pekee na kuepuka gharama kubwa ya kuagiza nje ya nchi.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja Mkuu wa Miradi ya Umeme ya TANESCO, Mhandisi Emmanuel Manirabona (kushoto)   kwenye ziara yake katika kituo cha kupoza umeme cha Kurasini kilichopo jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akitoa maelekezo kwa watendaji wa Shirika la  Umeme Tanzania (TANESCO) katika kituo cha kupoza umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kituo cha kupoza umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani pamoja na watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) akiendelea na ziara katika eneo la kituo kipya cha kupoza Umeme cha Kigamboni lililopo Dege jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Mbutu wilayani Kigamboni kwenye ziara hiyo




Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa kwenye ziara hiyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha kutengeneza mita za LUKU cha Ihemeter Tanzania Limited, Abraham Renakili (kulia) akielezea shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kutoka kulia).



Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha kutengeneza mita za LUKU cha Ihemeter Tanzania Limited, Abraham Renakili (kulia)



Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza mita za LUKU cha Ihemeter Tanzania Limited, Honoratha Kundi (aliyekaa) akielezea hatua za utengenezaji wa mita za LUKU kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyesimama kulia)



Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza mita za LUKU cha Ihemeter Tanzania Limited, wakiendelea na kazi.







COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI KALEMANI ATEMBELEA VITUO VYA KUPOZA UMEME DAR ES SALAAM NA KIWANDA CHA MITA CHA INHEMETER TANZANIA LIMITED
WAZIRI KALEMANI ATEMBELEA VITUO VYA KUPOZA UMEME DAR ES SALAAM NA KIWANDA CHA MITA CHA INHEMETER TANZANIA LIMITED
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj6tnwW8xNRcKbT6TVVr-9ki7aI4a2TbFtlnAPCPSQkYjqnE1guD_3SrXU-YHVC2p2EFCfXWuLvdoZhfzTfIZwbLL1665TBDiEe6gO_c8lRNo7-CzrnFjxhwLWuTO_I-R0LaD0I1cxe6V4/s640/PICHA+NA+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj6tnwW8xNRcKbT6TVVr-9ki7aI4a2TbFtlnAPCPSQkYjqnE1guD_3SrXU-YHVC2p2EFCfXWuLvdoZhfzTfIZwbLL1665TBDiEe6gO_c8lRNo7-CzrnFjxhwLWuTO_I-R0LaD0I1cxe6V4/s72-c/PICHA+NA+1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-kalemani-atembelea-vituo-vya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/waziri-kalemani-atembelea-vituo-vya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy