Na Samwel Mtuwa –DODOMA. Waziri wa Madini, Angellah Kairuki leo amekutana na balozi wa Japani nchini, Masaharu Yoshida mjini Dodoma l...
Na Samwel Mtuwa –DODOMA.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki leo amekutana na balozi wa Japani nchini, Masaharu Yoshida mjini Dodoma lengo likiwa ni kujadiliana namna ya kushirikiana kwenye uwekezaji wa madini nchini.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Kairuki alisema lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili maandalizi ya Jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini kati ya Tanzania na Japan.
Alisema kupitia jukwa hilo, wadau kutoka nchi zote mbili watafahamu fursa za uwekezaji katika sekta ya madini kama vile uongezaji thamani ya madini yapatikanayo nchini na namna ya kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo.
Kairuki aliongeza kuwa mbali na fursa mbalimbali katika sekta ya madini jukwaa hilo litaangalia namna ya kuongeza ajira kwenye sekta hiyo kwa kuwajengea uwezo wadau wa madini nchini.
Balozi Yoshida aliambatana na Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya uwekezaji katika sekta ya madini.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akiagana na Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida (kulia) mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho. |
COMMENTS