SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA NI MKOMBOZI WA WANANCHI
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
HomeUchumi

SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA NI MKOMBOZI WA WANANCHI

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma Serikali ilizindua sera ya Taifa ya huduma ndogo za fedha ili kuhakikisha wakopaji wakiwemo wajasiriama...


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali ilizindua sera ya Taifa ya huduma ndogo za fedha ili kuhakikisha wakopaji wakiwemo wajasiriamali wadogo wanalindwa na kupata haki zao bila kudhurumiwa wanapo hitaji mikopo na huduma zingine za kifedha zitakazowasaidia kujiendeleza kiuchumi.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge Mhe. Khatibu Said Haji aliyetaka kujua hatua za Serikali kuhusu taasisi za huduma ndogo za kifedha (Microfinance) kuwatoza wananchi riba kubwa wanapochukua mikopo.

Dkt. Kijaji, alisema kuwa  mwezi Desemba, 2017 Serikali ilizindua sera ya huduma ndogo ya fedha itakayosaidia  kuwatambua wakopeshaji  na kuwalinda wakopaji wanaohitaji huduma katika taasisi hizo zikiwemo za mikopo.

“Tunataka kuhakikisha tunawalinda wakopaji na kuhakikisha wanakopa kwa kuzingatia sheria na taasisi hizo za fedha zinazingatia sheria, utaratibu na kanuni za utawala bora”, alisema Dkt. Kijaji.

Alisema kukamilika kwa sheria ya huduma ndogo ya fedha hivi karibuni kutakua ni muarobaini wa kutatua changamoto za kifedha kwa wananchi wanaohitaji mikopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.

Akijibu swali la Msingi la Mbunge huyo kuhusu hatua za Serikali za kuhakikisha Benki nchini zinapunguza riba ili kuchochea shughuli za biashara, Dkt. Kijaji alisema kuwa Sekta ya Benki inafanya biashara huria na ilianza tangu mwaka 1991 baada ya kupitishwa kwa Sheria ya Usimamizi wa Benki na Vyombo vya Fedha ya Mwaka 1991.

“Kupitia Sheria hiyo, wawekezaji walifungua benki binafsi nchini na gharama za huduma na bidhaa kuamuliwa na nguvu ya soko hivyo Serikali haina mamlaka ya moja kwa moja ya kupunguza viwango vya riba katika soko”, alisisitiza Dkt. Kijaji.

Hata hivyo alizitaja hatua ambazo Serikali imezichukua kwa upande wake kuwa ni pamoja na kuzitaka benki za biashara kutumia Mfumo wa kuhifadhi na kutoa taarifa za wakopaji, Benki Kuu kuanza kutoa mikopo ya muda mfupi kwa benki za biashara kwa kiwango cha asilimia 6.89 na pia kushusha riba kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0.

Hatua zingine ni Benki Kuu kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa  na Benki za biashara  kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0  na pia Serikali kuendelea kulipa malimbikizo ya madai yaliyohakikiwa kwa lengo la kupunguza kiwango cha mikopo chechefu na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi.

Aidha Naibu Waziri huyo ameipongeza benki ya CRDB, NMB na Benki ya ABC kwa kupunguza riba ya mikopo kutoka asilimia zaidi ya 20 hadi kufikia asilimia 17 hivyo kuwa na tumaini kuwa Benki zingine zitaendelea kufanya hivyo.

Imetolewa na;
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA NI MKOMBOZI WA WANANCHI
SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA NI MKOMBOZI WA WANANCHI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjuF7GEFpx0yS8AsbI1l4m_mKvdMJRL1F9nLFkdjcMd0SFbOPfQ3JTuM6w3bCcYGnlOxg74ITliq9KiH8YUo_6W5laimKNl2gDiXaD6ANeX_FUQqQ7AsxadV2ngdZew5XjO8Kdb5tkojuk/s640/9132.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjuF7GEFpx0yS8AsbI1l4m_mKvdMJRL1F9nLFkdjcMd0SFbOPfQ3JTuM6w3bCcYGnlOxg74ITliq9KiH8YUo_6W5laimKNl2gDiXaD6ANeX_FUQqQ7AsxadV2ngdZew5XjO8Kdb5tkojuk/s72-c/9132.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/sera-ya-taifa-ya-huduma-ndogo-za-fedha.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/sera-ya-taifa-ya-huduma-ndogo-za-fedha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy