JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz ...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Mei, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli amepokea salamu kutoka kwa viongozi wa chama na Serikali wa Afrika Kusini na Zimbabwe ambako hivi karibuni Ndg. Kinana aliongoza ujumbe wa viongozi wa CCM kutembelea nchi hizo na kukutana na viongozi wakuu wa vyama tawala vya ANC na ZANU-PF vinavyoongoza Serikali.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli na Ndg. Kinana wamezungumzia maandalizi ya vikao vya Kamati Kuu ya CCM (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) vitakavyofanyika tarehe 28-29, Mei, 2018 Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Mei, 2018
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)) Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumapili Mei 27, 2018 |
COMMENTS