KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY YAANDAA HUDUMA ZA MATIBABU BURE KWA WAKAZI WA KEREGE JUMAPILI
Mkuu wa kitengo cha sheria, Ives Mlawi kutoka DTB akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu DTB kudhamini gharama za matibabu kwenye kambi ya matibabu ya bure iliyoandaliwa na Klabu ya Rotary ya Oyster Bay itakayofanyika eneo la Kerege wilayani Bagamoyo. Wa tatu (kulia) ni Rais wa Rotary Club ya Oysterbay, Alfred Woiso na wadau mbalimbali.
HomeJamii

KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY YAANDAA HUDUMA ZA MATIBABU BURE KWA WAKAZI WA KEREGE JUMAPILI

Mkuu wa kitengo cha sheria, Ives Mlawi kutoka DTB akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu DTB kudhamini gharama za matiba...

ASILIMIA 75% YA NCHI WANACHAMA WA INTERPOL, YAKUBALI KUJIUNGA KWA PALESTINA KATIKA TAASISI HIYO
WAZIRI DKT. TZEBA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA MBOLEA DAR ES SALAAM
SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017









Klabu ya Rotary ya Oyster Bay imeandaa kambi ya matibabu ya bure itakayofanyika eneo la Kerege wilayani Bagamoyo. Huduma hizo za matibabu zitatolewa siku ya Jumapili tarehe 27 Novemba katika shule ya Msingi ya Kerege.

Timu ya wataalamu wa afya kutoka Hospitali mbalimbali, wanafunzi wa udaktari, wanachama wa Rotary na wafanyakazi wa kujitolea kutoka sekta mbalimbali watashiriki katika kambi hiyo ya matibabu.

Vipimo na matibabu yatatolewa kwa magonjwa kama malaria, upungufu wa damu, kisukari na shinikizo la damu, masikio, pua na koo (ENT), magonjwa ya ngozi, macho, meno na kansa ya kizazi kwa akina mama. Miwani zitatolewa kwa watu watakaokutwa na matatizo ya macho. Huduma za ushauri kwa wajawazito zitatolewa na wajawazito pia watapatiwa vifaa vya kujifungulia bure.

Wakazi wa Kerege na maeneo ya jirani wanaombwa kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa hiyo ya matibabu ya bure haswa akina mama na watoto.

Akizungumza kuhusu mradi huu, Alfred Woiso, Rais wa Klabu ya Rotary ya Oyster Bay alisema, “Tuna furaha kuandaa kambi hii kwa mara nyingine tena kwa wakazi wa Kerege ambapo lengo letu ni kuwasaidia watu ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu. Tunawashukuru wadhamini na watu wote wanaojitolea katika mradi huu na tunakaribisha watu kuhudhuria na kusaidia kwa namna yoyote ile katika kambi hii ya matibabu.”

Usajili wa matibabu utaanza mapema asubuhi na watu wapatao 1,200 wanatarajiwa kupata huduma za matibabu kulingana na mwenendo wa idadi ya watu ambao huwa wanajitokeza kila mwaka kambi hiyo inapofanyika. Wakazi wa Kerege wanashauriwa kufika mapema ili kuweza kupata huduma.

Kambi hiyo ya matibabu imedhaminiwa na Diamond Trust Bank na inaandaliwa kwa ushirikiano na Shree Hindu Mandal Hospital, Vital Supplies, Whitedent, vClick Concepts Inc, MAK Books and Brains, ABACUS Pharmaceuticals, Fazel Foundation na wanachama wa Klabu ya Rotary na Rotaractor.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY YAANDAA HUDUMA ZA MATIBABU BURE KWA WAKAZI WA KEREGE JUMAPILI
KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY YAANDAA HUDUMA ZA MATIBABU BURE KWA WAKAZI WA KEREGE JUMAPILI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4PEw_pssWmlOICRUqFGVT7gnskJFnijn6pOt2bKW556ZanlSS92d1wSD5Qq9RYS03_Xgd8wMgj9z1WlZZC-2tUd3iQoN54xMOwGNXNY80VMUwOicZgb4g2qoyb2hrohRcQbCRw8mdhham/s640/DSC_0318.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4PEw_pssWmlOICRUqFGVT7gnskJFnijn6pOt2bKW556ZanlSS92d1wSD5Qq9RYS03_Xgd8wMgj9z1WlZZC-2tUd3iQoN54xMOwGNXNY80VMUwOicZgb4g2qoyb2hrohRcQbCRw8mdhham/s72-c/DSC_0318.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/klabu-ya-rotary-ya-oyster-bay-yaandaa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/klabu-ya-rotary-ya-oyster-bay-yaandaa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy