MAKAMU WA RAIS APOKEA VIFAA VYA UPASUWAJI WATOTO MNH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema uboreshaji wa huduma katika hospitali zet...










Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema uboreshaji wa huduma katika hospitali zetu za kibingwa kama MOI, zitaipunguzia Serikali mzigo wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi na hivyo kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kupokea vifaa vya Chumba Cha Upasuaji wa Watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI) leo tarehe 15 Mei, 2018.“ Aidha kwa namna ya kipekee nakushukuru Mheshimiwa Balozi wewe binafsi na Serikali ya Kuwait kwa ushirikiano ambao mnaendelea kuipatia Serikali yetu ya awamu ya Tano katika Sekta mbalimbali za maendeleo lakini hasa hasa katika sekta ya afya” alishukuru Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kuwa Balozi wa Kuwait Mhe. Jasem Al Najem amekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza sekta ya Afya hapa nchini ambapo leo wamesaidia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 258 ambavyo vitaiwezesha Taasisi kuimarisha utoaji wa huduma ya upasuaji hasa kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Makamu wa Rais amesema msaada huo utaiwezesha Taasisi kuwa na chumba cha upasuaji ambacho kitakuwa maalum kwa watoto tu, hivyo idadi ya wagonjwa watakaopata huduma ya upasuaji itaongezeka kutoka 500-700 kwa mwezi, kufikia zaidi ya wagonjwa 1000 kwa mwezi na watahudumiwa kwa haraka zaidi.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile  amesema Tanzania iatendelea kuimarisha uhusiano na nchi ya Kuwait kwani wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa msaada haswa msaada inayohusu sekta ya afya. Balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Al Najem amesema kuwa Wananchi wa Kuwait wana mapenzi makubwa na Watanzania na kuahidi wataendelea kutoa msaada.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsalimia mtoto Daniella Wilfred Pallangyo mwenye umri wa miaka 8 ambaye ana matatizo ya kichwa kikubwa wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa kuwait nchini Mhe. Jasem Al Najem wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI). 
 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI). 


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya baadhi ya vifaa vya upasuaji kutoka kwa Dkt. Karima Khaled wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI). 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya baadhi ya vifaa vya kisasa vya upasuaji vinavyoweza kuona mishipa na kuisoma kutoka kwa Dkt. Karima Khaled wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS APOKEA VIFAA VYA UPASUWAJI WATOTO MNH
MAKAMU WA RAIS APOKEA VIFAA VYA UPASUWAJI WATOTO MNH
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi4IZX7-9_DBCZwvz2wUyDYi1JJ7R9qFUfRW_57adRJ7BeIP9yn6c0TTSVdDL5id02BnuHIm05NO3yaieoP0_n7pp-5q6R9PYNkkG0POmXhTmMFtNQMGRCN_TeoyCyCmRer5qmnaopbl1U/s640/11.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi4IZX7-9_DBCZwvz2wUyDYi1JJ7R9qFUfRW_57adRJ7BeIP9yn6c0TTSVdDL5id02BnuHIm05NO3yaieoP0_n7pp-5q6R9PYNkkG0POmXhTmMFtNQMGRCN_TeoyCyCmRer5qmnaopbl1U/s72-c/11.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/makamu-wa-rais-apokea-vifaa-vya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/makamu-wa-rais-apokea-vifaa-vya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy