VIONGOZI KIVULE,DAR WAUNGANISHA NGUVU KUWASAKA VIBAKA DARAJANI
HomeJamii

VIONGOZI KIVULE,DAR WAUNGANISHA NGUVU KUWASAKA VIBAKA DARAJANI

  Daraja la Kivule likiendelea kujengwa katika Mto Kizinga eneo la Sirali,Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi wakipita kwenye daraja ...

MAKONDA APOKEA MAGODORO 1,000 NA KUSEMA SASA HAKUNA MGONJWA KULALA CHINI MKOANI DAR ES SALAAM
RC MAKONDA ARIDHISHWA NA UKARABATI MKUBWA WA MAGARI YA JESHI LA POLISI MKOA WA DAR ES SALAAM
U.S. EMBASSY GRADUATES ENGLISH LANGUAGE PROGRAM IN DAR ES SALAAM


 Daraja la Kivule likiendelea kujengwa katika Mto Kizinga eneo la Sirali,Dar es Salaam.

Baadhi ya wananchi wakipita kwenye daraja la muda baada lile la awali kubomolewa kupisha ujenzi wa daraja hilo jipya ambalo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi ujao. 


Na Richard Mwaikenda, Kivule, Dar


Viongozi wa Kata ya Kivule, Ukonga Dar, wameunganisha nguvu kuwasaka vipaka wanaowapora watu wanaopita wakati wa usiku katika Daraja linalojengwa katika MTO Kizinga.


Uamuzi huo umefanywa baada hivi karibuni Majira ya SAA 5 usiku ambapo mtu mmoja aliyekuwa akivuka katika Daraja la muda kuporwa na vibaka Simu na vitu vingine.


Tukio hili aliliripoti kituo kidogo cha POLISI cha Kitunda, na kwa viongozi wa Kata ya Kivule, akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kivule, Amos Angaya na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kerezange, Ismail Ibrahim.


Mwandishi wa Habari hii alishuhudia viongozi hao wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi, Kijana Jaffari aliyekamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika uporaji huo akishirikiana na wenzie.


Viongozi hao walimnasa 'Kibaka' huyo kwa ushirikiano Mkubwa na waendesha bodaboda pamoja na wafanyabiashara ndogondogo wanaoendesha shughuli zao darajani hapo.


Walimnasa Jaffari baada ya kutumia mbinu ya kuwatishia wanaoendesha shughuli zao darajani hapo kwamba wasipowataja vibaka basi wote watafukuzwa eneo hilo.


Walimnasa Jaffari baada ya kutumia mbinu ya kuwatishia wanaoendesha shughuli zao darajani hapo kwamba wasipowataja vibaka basi wote watafukuzwa eneo hilo.


Kwa umoja wao, viongozi hao waliapa kutokomeza vitendo vya uovu vilivyoanza kuota mizizi katika eneo hilo la Daraja ambalo limekata mawasiliano ya usafiri Kati ya Kivule Mwembeni na Silari baada Daraja bovu kuvunjwa na kuanza kujenga jipya.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kerezange, Ismail Ibrahim, Ujenzi wa Daraja hilo unatarajiwa kukamilika Mei, Mwaka huu.


Hivi sasa daladala kutoka Banana zinaishia upande wa Mwembeni na zinazotoka Frem kumi zinaishia Silari. Magari mengine yanapitia Daraja la Bombambili.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG. 0715264202,0689425467
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VIONGOZI KIVULE,DAR WAUNGANISHA NGUVU KUWASAKA VIBAKA DARAJANI
VIONGOZI KIVULE,DAR WAUNGANISHA NGUVU KUWASAKA VIBAKA DARAJANI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWsGpxzGm3c9OQ9ARrsOUWc-EVCT_7ksDduKb7D1abEZ-YDWfJYBqsnsAf82Nwv4_2zIy-Pd7Aqh1mwaxRGOOtZ8oAc0f2n_K-rfhhJ_JshT6u95a3txVBd45-82HD5bZsTiImDWgCG6de/s640/IMG_20180402_153916.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWsGpxzGm3c9OQ9ARrsOUWc-EVCT_7ksDduKb7D1abEZ-YDWfJYBqsnsAf82Nwv4_2zIy-Pd7Aqh1mwaxRGOOtZ8oAc0f2n_K-rfhhJ_JshT6u95a3txVBd45-82HD5bZsTiImDWgCG6de/s72-c/IMG_20180402_153916.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/viongozi-kivuledar-waunganisha-nguvu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/viongozi-kivuledar-waunganisha-nguvu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy