VIDEO; OPERESHENI YA POLISI YANASA SILAHA NA WAHALIFU
(Juu na chini) Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha baadhi ya Silaha zilizokamatwa katika Operesheni  maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu inayoendelea katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma. Wengine ni Maofisa mbalimbali waliopo katika Operesheni hiyo.
HomeJamii

VIDEO; OPERESHENI YA POLISI YANASA SILAHA NA WAHALIFU

SILA Na. Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kukamata Silaha mbalimbali na watuhumiwa 368 katika Oparesheni Maalum ...

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA KIKAO CHA MAAFISA WAANDAMIZI, MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI WA JESHI LA POLISI DAR
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAZISHI YA MAREHEMU MZEE FRANCIS MAIGE KANYASU
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU MKUU WA MKOA WA PWANI, ENG EVARIST NDIKILO



SILA
Na. Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kukamata Silaha mbalimbali na watuhumiwa 368 katika Oparesheni Maalum inayoendelea katika Ukanda wa Kusini unaojumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.


Akizungumza mkoani Mtwara, Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kati ya watuhumiwa 368, 13 tayari wamefikishwa Mahakamani, 152 wamekabidhiwa Idara ya Uhamiaji kwa hatua zaidi, tisa wapo chini ya Upelelezi na 194 wapo chini ya uangalizi wa Polisi (Police Supervisee).


Sabas amezitaja Silaha zilizokamatwa kuwa ni pamoja na SMG mbili, Pistol tano, Shotgun moja na risasi 145,  Visu 96, Makoti ya Sare za Jeshi la Msumbiji mawili, Raba za Jeshi la Msumbiji jozi mbili pamoja na vifaa vya kutengenezea milipuko.


“Baadhi ya watuhumiwa ni wale waliokimbia katika Operesheni yetu ya Mkoa wa Kipolisi Rufiji baada ya kuwazidi nguvu na sasa nawaambia tu wajisalimishe kwani hatuna mchezo hata wakimbilie wapi mana tumepata taarifa kuwa wamejificha nchini Msumbiji lakini kule napo wameanzisha operesheni kama hii“. Alisema Sabas.
Aidha Kamanda Sabas amesema Operesheni hiyo  ni endelevu na inashirikisha vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama hivyo ametoa wito kwa raia wema kuendelea kutoa taarifa za siri ili kuendeleza amani na usalama hapa nchini.


Hivi karibuni Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchini Msumbiji alikutana na IGP Simon Sirro jijini Dar es Salaam kwa lengo kuboresha ushirikiano katika mapambano ya uhalifu unaovuka mipaka ambayo ndio imekuwa changamoto katika nchi mbalimbali.

(Picha na Jeshi la Polisi).











Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VIDEO; OPERESHENI YA POLISI YANASA SILAHA NA WAHALIFU
VIDEO; OPERESHENI YA POLISI YANASA SILAHA NA WAHALIFU
https://i.ytimg.com/vi/0AthThnPQY4/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/0AthThnPQY4/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/video-operesheni-ya-polisi-yanasa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/video-operesheni-ya-polisi-yanasa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy