VIDEO; MAKAMU WA RAIS AHAMASISHA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO KATIKA ZIARA YA KIKAZI MJINI UNGUJA

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwapatia trekta moja wakulima wa mkoa wa Mjini Magharibi ili liweze kusaidia wakulima k...




Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwapatia trekta moja wakulima wa mkoa wa Mjini Magharibi ili liweze kusaidia wakulima kulima kwa wakati.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Mradi wa Wakulima wa Mpunga katika bonde la Kizimbani lililobo wilaya ya Magharibi A mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Makamu wa Rais aliwaambia wakulima hao kuwa Mjenga Nchi ni Mwanachi na aliwahimiza viongozi wote kuwa mstari wa mbele kwenye shughuli za kuleta maendeleo na kushirikiana bega kwa bega na wananchi.
Makamu wa Rais ambaye ameanza ziara ya siku nne ya kuhamasisha shughuli za maendeleo ya CCM Zanzibar, amewataka viongozi na wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi kushirikiana na kudumisha amani ya nchi.
Pamoja na kutembelea shamba la mpunga ambapo alisimamia zoezi la upandaji mpunga Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea eneo la Fuoni Kibaoni ambao alishuhudia upandwaji wa miti ya mikoko kwa kiasi kikubwa ikiwa shemu ya utunzaji wa mazingira lakini pia utunzaji na uzalishaji wa Kaa.
Katika ziara hiyo Makamu wa Rais aliambata na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Mabodi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ndugu Ayoub Mohammed Mahmoud pamoja na Viongozi wengine wa Chama na Serikali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya shamba la mpunga katika bonde la Kizimbani toka kwa Katibu wa Jumuiya ya Wakulima Kizimbani Bw. Shafii Kibwana Said ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo katika mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na na wenyeji wake alipotembelea shamba hilo ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo katika mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar. Kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Wakulima Kizimbani Bw. Shafii Kibwana Said






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuweka kaa kwenye maji kama ishara ya kuhamasisha utunzaji mazingira na uzalishaji wa katika eneo la Fuoni Kibondeni. 





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wanachama wa CCM wa Tawi la Fuoni Kibondeni mara baada ya kuweka jiwe la ujenzi wa Tawi hilo mkoa wa Mjini Magharibi.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VIDEO; MAKAMU WA RAIS AHAMASISHA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO KATIKA ZIARA YA KIKAZI MJINI UNGUJA
VIDEO; MAKAMU WA RAIS AHAMASISHA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO KATIKA ZIARA YA KIKAZI MJINI UNGUJA
https://i.ytimg.com/vi/APkyBe3cDVs/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/APkyBe3cDVs/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/video-makamu-wa-rais-ahamasisha.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/video-makamu-wa-rais-ahamasisha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy