TEWW KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUKUZA ELIMU NCHINI
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) , Dkt. Kassimu Nihuka akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)  juu ya dhana ya Elimu ya Sekondari nje ya mfumo rasmi, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Karibu Tanzania Organization (KTO), Maggid Mjengwa. 
HomeJamii

TEWW KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUKUZA ELIMU NCHINI

Na Mwandishi Wetu Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeandaa mafunzo ya siku tano ili kuwajeng...

WAZIRI DK.CHARLES TIZEBA KUFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA KILIMO JIJINI DAR ES SALAAM KESHO
TAKWIMU ZINAZOONESHA HALI YA UZAZI SALAMA NCHINI TANZANIA
MEYA ILALA AFUNGUA RASMI DARAJA LA BONYOKWA-KINYEREZI
Na Mwandishi Wetu

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeandaa mafunzo ya siku tano ili kuwajengea uwezo walimu 30 kutoka vyuo vya Maendeleo ya Wananchi hapa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na  TEWW Jijini Dar es Salaam, Programu hii ijulikanayo kama “ Elimu Haina Mwisho- Skills Development Program For Young Women Through Folk Development Colleges ” inalenga kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.
Sehemu ya taarifa hiyo imeeleza kuwa programu hiyo imegawanyika katika awamu mbili na inalenga  Wanawake na Vijana ambao wamekatishwa masomo kwasababu mbalimbali ikiwamo mimba za utotoni.
“ Mafunzo haya yanaandaliwa na Karibu Tanzania Organization (KTO) kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) pamoja na Taasisi ya Aflatoun International ya Uholanzi na Wakfu wa Mastercard(Mastercard Foundation) “ Imesisitiza sehemu ya taarifa hiyo.
Mafunzo yanayotolewa ni ya miaka miwili ikiwamo elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi, ujasiriamali, stadi za maisha na ufundi.
Jukumu hili linaendana na jukumu la kisheria la TEWW la kuandaa na kutoa mafunzo kwa walimu, wawezeshaji na wasimamizi wa elimu ya watu wazima nchini. Washiriki wa mafunzo haya ni wakufunzi  wa vyuo vitatu vya maendeleo ya wananchi  (FDC) nchini kutoka Mbinga FDC (Ruvuma), Bigwa FDC (Morogoro) na Masasi FDC (Mtwara).
Pia taarifa hiyo imebainisha kuwa Watakapomaliza mafunzo hayo, wakufunzi  hao waliojengewa uwezo watarudi kufundisha kwenye vyuo vyao,  Programu ni ya miaka minne na inalenga kuvifikia vyuo vyote 55. Wanawake Vijana 10,000 watanufaika na program hii. 
 TEWW ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Namba 12 yamwaka 1975 na kupewa majukumu mbalimbali. Pamoja na majukumu mengine, Taasisi inajukumu la kutoa elimu ya sekondari kwanjia ya Ujifunzaji Huria na Masafa (UHM) pamoja na kuandaa wataalamu wa elimu ya watu wazima na Maendeleo ya Jamii .
Asasi  ya KTO  inayofanya kazi pamoja na vyuo vyote 55 vya Maendeleo ya Wananchi kwenye kutekeleza programu mbalimbali kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu  Sayansi na Teknolojia na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi. 
Programu hii yenye kuwalenga Wanawake Vijana itakuwa njia mbadala ya kuwasaidia walengwa kwenye kusonga mbele kwenye maisha na kuchangia kwenye kuinua uchumi wa Taifa ilikuifikisha Tanzania ya viwanda, hivyo TEWW na KTO imeandaa mafunzo kwa waalimu wa vyuo vya maendeleo ya Wananchi ili kuwajengea uwezo wa namna ya kuendesha programu hii.
Aidha kwa kushirikiana na KTO Kaimu Mkurugenzi wa TEWW Dkt. Kassimu Nihuka amefafanua kuwa, TEWW  kupitia programu hii inatoa fursa  kwa wanawake vijana waliokatisha elimu yao kwasababu mbalimbali ikiwamo ndoa za utotoni, kukimbia ukeketaji na hata kukatishwa masomo yao kwa ujauzito kupata elimu mbadala.
Elimu hiyo itatolewa katika maeneo ya ufundi,stadi za maisha, stadi za fedha, ujasiriamali na elimu ya Sekondari. Utolewaji wa mafunzo hayo itasaidia kupanua soko la ajira ikiwamo uwezo wa kuajiriwa, kujiajiri na kupata sifa ya kuendelea zaidi na masomo.

Hivyo, programu hii inawalenga Wanawake Vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu ili wapate fursa ya kupata elimu ya mafunzo ya ufundi, ujasiriamali na elimu ya Sekondari. Kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Karibu Tanzania Organization wamekusudia kwa dhati  kuboresha maisha ya wanawake vijana waliokosa fursa katika mfumo rasmi ili waweze kujiajiri au kuajiriwa hivyo kuboresha maisha yao na kuchangia katika uchumi wa Taifa.

Aidha, Mkurugenzi wa KTO alisema kuwa programu hii imeshirikisha Shirika lisilo la kiserikali la Uholanzi la Aflatoun International na  Mfuko wa wakfu wa Kimataifa wa Mastercard (Mastercard Foundation)

 KTO kwa kushirikiana na TEWW inawakaribisha wote kujiunga na programu hii itakayotekelezwa kwa kuanzia kwenye Vyuo Vya  Maendeleo ya wananchi vya  Mbinga, Masasi na Bigwa kwa mwaka 2018.  Mkurugenziwa KTO, Bw. Maggid Mjengwa ameyasema hayo  leo jijini Dar es Salaam, wakati wa kufunga mafunzo kwa Wakufunzi wa Vyuo vya MaendeleoyaWananchi.
Karibu Tanzania Organization (KTO) kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) pamoja na Taasisi ya Aflatoun International ya Uholanzi na Wakfu wa Mastercard(Mastercard Foundation) imeandaa mafunzo ya siku tano ili kuwajengea uwezo walimu 30 kutoka Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi. Programu hii ijulikanayo kama – Elimu Haina Mwisho- Skills Development Program For Young Women Through Folk Development Colleges.


Mkurugenzi wa Karibu Tanzania Organization (KTO), Bw. Maggid Mjengwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu majukumu ya KTO na maeneo ya ushirikiano na TEWW.  Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya KTO, Aidan Mchawa na kulia Kaimu Mkurugenzi wa TEWW Dkt. Kassimu Nihuka. 

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu toka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Happiness Magoma akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) mchango wa Wizara hiyo katika miradi ya KTO. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TEWW Dkt. Kassimu Nihuka. (Picha zote na Leondard Lupeja-TEWW)




Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TEWW KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUKUZA ELIMU NCHINI
TEWW KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUKUZA ELIMU NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhtXuBa5N-sIw960pOscRp-cfsZOQ8mHEjTk2KPV6OvqHgIYmYJe6iwKYI2Muphs_gg4UMuuikp77WUdUEQiqr9Jka3tBpYAoG3961lpABA3hKWMqfVrmvDYeEk327-H2xTW3G4W8Ghevc/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhtXuBa5N-sIw960pOscRp-cfsZOQ8mHEjTk2KPV6OvqHgIYmYJe6iwKYI2Muphs_gg4UMuuikp77WUdUEQiqr9Jka3tBpYAoG3961lpABA3hKWMqfVrmvDYeEk327-H2xTW3G4W8Ghevc/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/teww-kuendelea-kushirikiana-na-wadau.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/teww-kuendelea-kushirikiana-na-wadau.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy